عَن أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيَّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«إِذَا وُضِعَتِ الجِنَازَةُ وَاحْتَمَلَهَا الرِّجَالُ عَلَى أَعْنَاقِهِمْ فَإِنْ كَانَتْ صَالِحَةً قَالَتْ: قَدِّمُونِي، وَإِنْ كَانَتْ غَيْرَ صَالِحَةٍ قَالَتْ: يَا وَيْلَهَا أَيْنَ يَذْهَبُونَ بِهَا؟ يَسْمَعُ صَوْتَهَا كُلُّ شَيْءٍ إِلَّا الإِنْسَانَ، وَلَوْ سَمِعَهُ صَعِقَ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 1314]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudry -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Likiwekwa Jeneza, na wanaume wakalibeba katika shingo zao, likiwa ni la mtu mwema basi husema: Niwahisheni, na likiwa si la mtu mwema basi husema: Ubaya ulioje, mnalipeleka wapi? Huisikia sauti yake kila kitu isipokuwa mwanadamu, na lau angelisikia basi angezimia".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 1314]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba Jeneza likiwekwa kitandani, na wanaume wakalibeba katika shingo zao, likiwa ni la mtu mwema basi husema: Niwahisheni, kwa yale linayoyaona mbele yake katika neema, na likiwa si la mtu mwema, hupiga yowe kwa sauti mbaya ya kukera, na kusema: Nasikitika kwa maangamivu yake, mnalipeleka wapi?! kwa yale linayoyaona mbele yake miongoni mwa adhabu, inasikika sauti yake kwa kila kitu isipokuwa mwanadamu, na lau angeliisikia basi angezimia kutokana na ukubwa wa kile alichosikia.