+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ:
«إِذَا جَاءَ رَمَضَانُ فُتِّحَتْ أَبْوَابُ الْجَنَّةِ، وَغُلِّقَتْ أَبْوَابُ النَّارِ، وَصُفِّدَتِ الشَّيَاطِينُ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 1079]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Inapokuja Ramadhani hufunguliwa milango ya pepo na hufungwa milango ya moto, na mashetani hufungwa minyororo".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 1079]

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa unapoingia mwezi wa Ramadhani hutokea mambo matatu: La kwanza: Hufunguliwa milango ya pepo na haufungwi mlango wowote katika milango hiyo. La pili: Hufungwa milango ya moto na haufunguliwi mlango wowote katika hiyo. La tatu: Hufungwa minyororo mashetani na majini wakaidi, hawaachwi kuendelea na yale waliyokuwa nayo katika miezi mingine isiyokuwa Ramadhani. Na yote hiyo ni kwa kuutukuza mwezi wa Ramadhani, na kumhamasisha mtendaji kukithirisha ibada, kama swala na sadaka, na dhikiri na kusoma Qur'ani na mengineyo; na kujitenga mbali na madhambi na maasi.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kiassam الهولندية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Fadhila za mwezi wa Ramadhani.
  2. Habari njema kwa wafungaji ndani yake kuwa mwezi huu mtukufu ni msimu wa ibada na kheri.
  3. Katika kufungwa mashetani ndani ya Ramadhani ni ishara ya kuondolewa udhuru kwa kila aliyelazimishwa kutekeleza sheria na ni kana kwamba anamwambia:
  4. Amesema Al-Qurtubi: Ikiwa patasemwa: Inakuwaje tunaona shari na maasi yanatokea ndani ya Ramadhani kwa wingi, na kama mashetani yangefungwa basi tusingeona? Jawabu: Ni kuwa maasi hupungua kwa wafungaji swaumu ambayo zimehifadhiwa sharti zake na zikazingatiwa adabu zake, au nikuwa wanaofungwa ni baadhi ya mashetani nao ni wale wakaidi na si wote kama ilivyotangulia katika baadhi ya riwaya, au makusudio yake ni kupungua kwa shari ndani yake, na jambo hili linaonekana, kwani kutokea kwake ni mara chache kuliko miezi mingine, kwani si lazima kufungwa wote kuwa kusitokee shari wala maasi; kwa sababu hilo lina sababu zingine zisizokuwa mashetani kama nafsi chafu na mazoea mabaya na mashetani wa kibinadamu.