عن أبي قتادة رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «من سَرَّهُ أَن يُنَجِّيَه الله من كَرْبِ يوم القيامة، فَلْيُنَفِّسْ عن مُعْسِر أو يَضَعْ عنه».
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abii Qatada -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayependa Mwenyezi Mungu amuokoe na Matatizo ya siku ya kiyama, basi amtatulie shida mwenye ugumu au ampunguzie"
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Maana ya hadithi: "Atakayependezwa" Yaani: atakayefurahishwa na akastaajabishwa. "Mwenyezi Mungu amuokoe na matatizo ya siku ya kiyama" Yaani: amuepushe kutokana na matatizo na mitihani ya siku ya kiyama. "Basi amtatulie shida mwenye ugumu" yaani amcheleweshe kumdai deni lake pale unapofikia muda na ampe muda mpana mpaka atakapopata cha kulipa deni lake. "Au ampunguzie" Yaani: amsamehe deni analomdai, lote au baadhi yake, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na iwapo mdaiwa hawezi kulipa basi mpeni muda, na ikiwa mtatoa sadaka (mtasamehe) ni bora kwenu ikiwa nyinyi mnajua".

Kufanya Tarjama: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibaghali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno
Kuonyesha Tarjama
Ziyada