عَنْ عُبَادَةَ بْنِ الصَّامِتِ رَضيَ اللهُ عنهُ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«فِي الجَنَّةِ مِائَةُ دَرَجَةٍ مَا بَيْنَ كُلِّ دَرَجَتَيْنِ كَمَا بَيْنَ السَّمَاءِ وَالأَرْضِ، وَالْفِرْدَوْسُ أَعْلاَهَا دَرَجَةً وَمِنْهَا تُفَجَّرُ أَنْهَارُ الجَنَّةِ الأَرْبَعَةُ، وَمِنْ فَوْقِهَا يَكُونُ العَرْشُ، فَإِذَا سَأَلْتُمُ اللَّهَ فَسَلُوهُ الفِرْدَوْسَ».
[صحيح] - [رواه الترمذي] - [سنن الترمذي: 2531]
المزيــد ...
Kutoka kwa Ubaada bin Swaamit radhi za Allah ziwe juu yake hakika Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Peponi kuna daraja mia moja baina ya kila daraja mbili ni kama umbali wa mbingu na ardhi, na Firdausi iko daraja ya juu zaidi kuliko zote, na ndani yake ndiko inako chimbuka mito yote minne ya pepo, na juu yake ndiko inakokuwa Arshi, Mkimuomba Allah basi muombeni Firdausi".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy] - [سنن الترمذي - 2531]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa peponi kuna daraja na vituo mia moja, na masafa yaliyopo kati ya daraja mbili ni kama masafa kati ya mbingu na ardhi, na Pepo ya juu zaidi miogongoni mwa Pepo hizi ni Pepo ya Firdausi, na ndani yake ndiko inapochimbuka mito yote minne ya Pepo, na juu ya Firdausi ndiko inakokuwa Arshi; mkimuomba Mwenyezi Mungu basi muombeni Firdausi; kwani ndiyo iko juu ya Pepo zote.