عَنْ جُنْدُبِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ:
كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَنَحْنُ فِتْيَانٌ حَزَاوِرَةٌ، فَتَعَلَّمْنَا الإِيمَانَ قَبْلَ أَنْ نَتَعَلَّمَ القُرْآنَ، ثُمَّ تَعَلَّمْنَا القُرْآنَ، فَازْدَدْنَا بِهِ إِيمَانًا.
[صحيح] - [رواه ابن ماجه] - [سنن ابن ماجه: 61]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Jundubu bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Tulikuwa pamoja Mtume rehema na amani ziwe juu yake nasi tukiwa vijana karibu na balehe, tukajifunza imani kabla ya kujifunza Qur'ani, kisha tukajifunza Qur'ani, tukaongeza imani kupitia Qur'ani.
[Sahihi] - [Imepokelewa na Ibnu Maajah] - [سنن ابن ماجه - 61]
Amesema Jundubu bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake: Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake nasi tukiwa vijana tuliokaribia kubalehe, wenye nguvu na wakali, tukajifunza kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake imani kabla ya kujifunza Qur'ani, kisha tukajifunza Qur'ani; tukazidisha imani kupitia Qur'ani.