عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«مَا مِنَ الأَنْبِيَاءِ نَبِيٌّ إِلَّا أُعْطِيَ مَا مِثْلهُ آمَنَ عَلَيْهِ البَشَرُ، وَإِنَّمَا كَانَ الَّذِي أُوتِيتُ وَحْيًا أَوْحَاهُ اللَّهُ إِلَيَّ، فَأَرْجُو أَنْ أَكُونَ أَكْثَرَهُمْ تَابِعًا يَوْمَ القِيَامَةِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 4981]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake:
"Hakuna yeyote katika Manabii isipokuwa alipewa mfano wa yale waliyoyaamini watu, na hakika niliyopewa mimi ni wahyi (ufunuo) wa Mwenyezi Mungu alionifunulia, basi nataraji kuwa na wafuasi wengi kuliko wao siku ya Kiyama".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 4981]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Manabii wote Mwenyezi Mungu aliwapa nguvu na akawapa alama na miujiza iliyo nje na kawaida ya watu, watakayoitumia kama ushahidi juu ya unabii wao na kumpelekea kuamini atakayeishuhudia kwa kuwasadikisha, na kwamba yeye ameshindwa katika changamoto hiyo, kiasi kwamba hawezi kuizuia yeye mwenyewe binafsi, lakini anaweza kupinga akakaidi. Bali yeye rehema na amani ziwe juu yake alama yake na muujiza wake ni Qur'ani aliyomteremshia Mwenyezi Mungu kwa Wahyi; kwa namna ilivyokusanya miujiza ya wazi tena endelevu kwa wingi wa faida zake na kuenea kwa manufaa yake, kwa kukusanya kwake ujumbe na hoja na habari za yale yatakayotokea, manufaa yake yakamuenea aliyepo na asiyekuwepo na aliyepatikana na atakayepatikana, kisha akasema: Basi ninataraji kuwa na wafuasi wengi zaidi yao siku ya Kiyama.