+ -

عَنْ قَتَادَةَ قَالَ:
سُئِلَ أَنَسٌ كَيْفَ كَانَتْ قِرَاءَةُ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ؟ فَقَالَ: «كَانَتْ مَدًّا»، ثُمَّ قَرَأَ: {بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ} [الفاتحة: 1] يَمُدُّ بِبِسْمِ اللَّهِ، وَيَمُدُّ بِالرَّحْمَنِ، وَيَمُدُّ بِالرَّحِيمِ.

[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 5046]
المزيــد ...

Kutoka kwa Katada amesema:
Aliulizwa Anasi kilikuwa vipi kisomo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake? Akasema: "Kilikuwa ni kuvuta", kisha akasoma: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu" [Al-Faatiha:1] Alikuwa akivuta neno: Bismillaahi, na anavuta Al-Rahmaani, na anavuta neno: Al-Rahiim.

[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 5046]

Ufafanuzi

Aliulizwa Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake kilikuwa vipi kisomo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika Qur'ani? Akasema: Alikuwa akivuta sauti yake kwa kisomo; akivuta herufi Lamu ilioko kabla ya "Haa" katika neno: "Allah", na anavuta herufi "Mim" ilioko kabla ya "Nuun" katika neno "Al-Rahmaan", na anavuta herufi "Haa" katika neno "Al-Rahiim".

Katika Faida za Hadithi

  1. Kuvuta ni kuzishibisha herufi za mada nazo ni (Alif, Wau, Yaa) zinapokuwa na sakina na kabla yake kukawa haraka (silabi) inayoendana nayo.
  2. Kumebainishwa muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kuisoma Qur'ani.
  3. Kutekeleza kwa vitendo kwa ajili ya kubainisha kisomo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  4. Amesema Assindi: Kauli yake: "Akivuta sauti yake", yaani anarefusha herufi zinazofaa kurefushwa kwa kuzitumia kuzingatia na kutafakari na kumkumbusha mwenye kukumbuka.
  5. Umuhimu wa kujua kanuni za kusoma Qur'ani (Tajwidi) na elimu za Qur'ani.
  6. Kuzielewa dalili kunarejeshwa kwa wanachuoni, kama alivyoulizwa Anasi radhi za Allah ziwe juu yake akambainishi muulizaji.
Tafsiri: Lugha ya Kiindonesia Kibangali Kivetenamu Kikurdi Kihausa Kireno Thai Kiassam الهولندية الدرية المجرية الجورجية المقدونية
Kuonyesha Tarjama