عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ السُّلَمي رحمه الله قَالَ:
حَدَّثَنَا مَنْ كَانَ يُقْرِئُنَا مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُمْ كَانُوا يَقْتَرِئُونَ مِنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَشْرَ آيَاتٍ، فَلَا يَأْخُذُونَ فِي الْعَشْرِ الْأُخْرَى حَتَّى يَعْلَمُوا مَا فِي هَذِهِ مِنَ الْعِلْمِ وَالْعَمَلِ، قَالُوا: فَعَلِمْنَا الْعِلْمَ وَالْعَمَلَ.

[حسن] - [رواه أحمد]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Abdulrahman Al-Sulamiy- Mwenyezi Mungu amrehemu amesema:
Ametusimulia mmoja miongoni mwa waliokuwa wakitusomea Qur'ani katika Maswahaba wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- walikuwa wakitusomea Aya kumi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, hivyo hawakuwa wakichukua Aya kumi zingine mpaka wawe wamekwishayafanyia kazi yaliyo ndani ya aya hizo kumi kwa kujifunza na kuyafanyia kazi, wakasema: Basi tukajifunza elimu na kuifanyia kazi.

Ni nzuri - Imepokelewa na Ahmad

Ufafanuzi

Walikuwa Maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- wakipokea Aya kumi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na hawakuwa wakihama kwenda Aya zingine mpaka wawe wamekwishajifunza elimu liyopo kwenye hizo Aya kumi, na wanazifanyia kazi, hivyo wakajifunza elimu pamoja na kuifanyia kazi.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Kibangali Kichina Kifursi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Ubora wa Maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, na pupa yao ya kujifunza Qur'ani.
  2. Kujifunza Qur'ani kunakuwa kwa kujifunza na kufanyia kazi yaliyopo ndani yake na kuyafanyia kazi, na siyo kuisoma na kuihifadhi peke yake.
  3. Elimu inakuwa kabla ya maneno na vitendo.
Ziada