+ -

عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«مَا مِنْ نَبِيٍّ بَعَثَهُ اللهُ فِي أُمَّةٍ قَبْلِي إِلَّا كَانَ لَهُ مِنْ أُمَّتِهِ حَوَارِيُّونَ، وَأَصْحَابٌ يَأْخُذُونَ بِسُنَّتِهِ وَيَقْتَدُونَ بِأَمْرِهِ، ثُمَّ إِنَّهَا تَخْلُفُ مِنْ بَعْدِهِمْ خُلُوفٌ يَقُولُونَ مَا لَا يَفْعَلُونَ، وَيَفْعَلُونَ مَا لَا يُؤْمَرُونَ، فَمَنْ جَاهَدَهُمْ بِيَدِهِ فَهُوَ مُؤْمِنٌ، وَمَنْ جَاهَدَهُمْ بِلِسَانِهِ فَهُوَ مُؤْمِنٌ، وَمَنْ جَاهَدَهُمْ بِقَلْبِهِ فَهُوَ مُؤْمِنٌ، وَلَيْسَ وَرَاءَ ذَلِكَ مِنَ الْإِيمَانِ حَبَّةُ خَرْدَلٍ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 50]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Hakuna Nabii aliyetumwa na Mwenyezi Mungu katika umma wowote kabla yangu, isipokuwa kunakuwa katika umma wake na watu wake wapendwa na watu wanaoyachukua mafundisho yake na wanafuata amri yake, kisha wanakuja kutofautiana baada yao watu wanaowafuata, wanazungumza yale wasiyoyafanya, na wanafanya ambayo hawakuamrishwa, atakayepigana nao kwa mkono wake basi huyo ndio muumini, na atakayepigana nao kwa moyo wake basi naye ni muumini, na atakayepigana nao kwa ulimi wake basi naye ni muumini, na hakuna zaidi ya hapo katika imani punje ndogo ya Haradali" (yaani kwa asiyefanya hivyo hana imani hata punje ndogo).

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 50]

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa hakuna Nabii aliyetumwa na Mwenyezi Mungu kwa umma kabla yake isipokuwa huwa na watu safi na watetezi, na mujahidina wa kweli kutoka katika umma wake wanaofaa kwa ukhalifa (uongozi) baada yake, wanaofuata Sunna zake na kufuata amri yake, kisha baada ya hao watangulizi wema wanakuja watu ambao hawana kheri ndani yake; Wanasema wasiyoyafanya, na wanafanya yale ambayo hawakuamrishwa kuyafanya, na atakayepigana nao kwa mkono wake basi huyo ni Muumini, atakayepigana nao kwa ulimi wake pia ni Muumini, na atakayepigana nao kwa moyo wake pia ni Muumini, na hakuna imani hata chembe ya haradali (ulezi) baada yake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai German Pashto Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية الرومانية Luqadda malgaashka الفولانية Luqadda Oromaha
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Himizo la kupambana na wanaokwenda kinyume na sheria kwa kauli zao na vitendo vyao.
  2. Moyo kutokukemea uovu ni dalili ya udhaifu wa imani au kutoweka kwake.
  3. Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwafanyia wepesi Manabii kuwapata wenye kubeba ujumbe wao baada yao.
  4. Atakayetaka kusalimika basi anatakiwa kufuata njia ya Manabii; kwa sababu kila njia isiyokuwa njia yao ni maangamivu na upotovu.
  5. Kila zama zinavyozidi kuwa mbali na Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Masahaba zake radhi za Allah ziwe juu yao watu huzidi kuacha mafundisho na kufuata matamanio na kuzusha mambo ya uzushi.
  6. Kumebainishwa daraja za Jihadi, nakuwa ni kwa mkono kwa mwenye kuweza kuuondoa uovu, kama wasimamizi na viongozi na watawala, na kwa kauli inakuwa kwa kubainisha haki na kuwalingania watu, na kwa moyo inakuwa kwa kuukemea uovu na kutoupenda au kuuridhia.
  7. Ulazima wa kuamrisha mema na kukataza uovu.