+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«إِنَّ أَوَّلَ زُمْرَةٍ يَدْخُلُونَ الجَنَّةَ عَلَى صُورَةِ القَمَرِ لَيْلَةَ البَدْرِ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ عَلَى أَشَدِّ كَوْكَبٍ دُرِّيٍّ فِي السَّمَاءِ إِضَاءَةً، لاَ يَبُولُونَ وَلاَ يَتَغَوَّطُونَ، وَلاَ يَتْفِلُونَ وَلاَ يَمْتَخِطُونَ، أَمْشَاطُهُمُ الذَّهَبُ، وَرَشْحُهُمُ المِسْكُ، وَمَجَامِرُهُمْ الأَلُوَّةُ الأَنْجُوجُ، عُودُ الطِّيبِ وَأَزْوَاجُهُمُ الحُورُ العِينُ، عَلَى خَلْقِ رَجُلٍ وَاحِدٍ، عَلَى صُورَةِ أَبِيهِمْ آدَمَ، سِتُّونَ ذِرَاعًا فِي السَّمَاءِ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 3327]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Hakika kundi la kwanza la watu watakaoingia peponi watakuwa katika sura ya mwezi usiku wa tarehe kumi na tano, kisha wale wanaowafuata watakuwa katika sura ya nyota kali ing'aayo na iangazayo mbinguni, hawatokwenda haja ndogo wala kubwa, na wala hawatotema mate wala kupenga kamasi, vitana vyao vitakuwa vya dhahabu, jasho lao litakuwa ni miski, na vitezo vyao vitakuwa vikinukia udi wenye harufu nzuri mno, udi wa marashi, na wake zao watakuwa ni katika Mahurulaini, na wote watakuwa katika umbile la mtu mmoja, watakuwa katika sura ya baba yao Adam, urefu kwenda juu ni dhiraa sitini (Dhiraa moja ni inchi 18)".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 3327]

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kundi la kwanza la waumini watakaoingia peponi nyuso zao zitakuwa na sura ya mwezi unapokuwa usiku wa tarehe kumi na tano katika mg'ao, kisha wale wanaowafuata watakuwa katika sura ya nyota kali yenye mng'ao na mwangaza katika mbingu, watakuwa na sifa za ukamilifu kiasi kwamba hawatokojoa, wala kujisaidia haja kubwa, na wala hawatotema mate wala kupenga kamasi, vitana vyao ni vya dhahabu, na jasho lao ni miski, na vitezo vyao vitakuwa vinafuka hurufu nzuri mno, na udi mzuri zaidi, na wake zao watakuwa ni Mahurulaini, umbile lao litakuwa kama umbile la mtu mmoja, watakuwa katika sura ya baba yao Adam katika urefu na umbile; ulikuwa urefu wa mwili wake ni dhiraa sitini kwenda juu.

Tafsiri: Lugha ya Kiindonesia Kivetenamu Kihausa Kiassam الأمهرية الهولندية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumebainishwa sifa za watu wa peponi, na kwamba wao wanatofautiana ndani yake kulingana na daraja zao na matendo yao.
  2. Kutumia mfumo wa kufananisha katika kusogeza karibu maana na kuifafanua.
  3. Amesema Qurtubi: Huenda mtu anaweza kusema kuna haja gani ya wao kuwa na machanuo hali yakuwa wameumbwa upya na nywele zao hazichafuki? Na wana haja gani ya wao kuwa na udi na hali yakuwa harufu yao ni nzuri kuliko miski? Akasema: Na linajibiwa hilo kuwa: Neema za watu wa peponi kama kula na kunywa na kuvaa na marashi hivi vyote havitakuwa kwa sababu ya maumivu ya njaa au kiu au uchi au harufu mbaya, bali ni ladha mfululuzo na neema mfululuzo, na hekima katika hilo nikuwa wao wataneemeka kwa aina mbali mbali ambazo walikuwa wakineemeka nazo katika dunia.