عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«نَحْنُ آخِرُ الأُمَمِ، وَأَوَّلُ مَنْ يُحَاسَبُ، يُقَالُ: أَيْنَ الأُمَّةُ الأُمِّيَّةُ وَنَبِيُّهَا؟ فَنَحْنُ الآخِرُونَ الأَوَّلُونَ».
[صحيح] - [رواه ابن ماجه] - [سنن ابن ماجه: 4290]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao -ya kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
"Sisi ni Umma wa mwisho, na ndio wa kwanza kuhesabiwa, patasemwa: Uko wapi Umma usiosoma na Nabii wao? Sisi ni wa mwisho wa mwanzo".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Ibnu Maajah] - [سنن ابن ماجه - 4290]
Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Umma wake ndio Umma wa mwisho kuwepo na zama pia, na ndio Umma wa kwanza katika Umma zote utakaohesabiwa siku ya Kiyama, patasemwa siku ya Kiyama: Uko wapi Umma usiosoma na Nabii wao? Umenasibishwa katika kutojua kusoma kwake rehema na amani ziwe juu yake kwa kutojua kusoma wala kuandika. Wataanza kuitwa mwanzo kwa ajili ya hesabu, sisi ni wa mwisho katika zama za kuwepo, na wa kwanza katika kuhesabiwa siku ya Kiyama na katika kuingia Peponi.