+ -

عَنْ أُبَيِّ بْنِ كَعْبٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«لاَ تَسُبُّوا الرِّيحَ، فَإِذَا رَأَيْتُمْ مَا تَكْرَهُونَ فَقُولُوا: اللَّهُمَّ إِنَّا نَسْأَلُكَ مِنْ خَيْرِ هَذِهِ الرِّيحِ وَخَيْرِ مَا فِيهَا وَخَيْرِ مَا أُمِرَتْ بِهِ، وَنَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ هَذِهِ الرِّيحِ وَشَرِّ مَا فِيهَا وَشَرِّ مَا أُمِرَتْ بِهِ».

[صحيح] - [رواه الترمذي] - [سنن الترمذي: 2252]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Ubaiyya bin Kaab -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Msiutukane upepo, mkiona yanayo kuchukizeni katika upepo basi semeni: Ewe Allah tunaomba kheri za upepo huu na kheri zilizomo, na kheri ambazo kwazo umeamrishwa upepo huu, na tunataka hifadhi na ulinzi kutokana na shari zake ,na shari ambazo kwa sababu yake umeamrishwa".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy] - [سنن الترمذي - 2252]

Ufafanuzi

Amekataza rehema na amani ziwe juu yake kuutukana au kuulani upepo, kwani umeamrishwa kutoka kwa muumba wake, huja kwa rehema na adhabu, na kuutukana ni kumtukana Mwenyezi Mungu muuba wake, na kuchukia maamuzi yake, kisha akaelekeza rehema na amani ziwe juu yake kurejea kwa Mwenyezi Mungu muumba wake kwa kumuomba kheri zake na kheri zilizo ndani yake, na kheri za yale yaliyotumwa, kama kuleta mvua na kuchevusha mimea na mfano wake, na kuomba kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake na shari zilizo ndani yake, na shari zilizotumwa, kama kuharibu mimea na miti na kuangamiza mifugo na kubomoa majengo, na mfano wake, na katika kumuomba Mwenyezi Mungu hilo kuna kutimiza na kuthibitisha kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Thai Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الرومانية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Katazo la kutukana upepo; kwa sababu ni kiumbe kilichopangiliwa, hapo matusi yanarudi kwa muumbaji wake na mpangiliaji wake, nayo ni mapungufu katika tauhidi.
  2. Kurejea kwa Mwenyezi Mungu na kuomba kinga kwake kutokana na shari ya vile alivyoumba.
  3. Upepo huamrishwa kwa kheri, na huamrishwa kwa shari.
  4. Amesema bin Baazi: Kuutukana upepo ni miongoni mwa maasi; kwa sababu ni kiumbe kilichopangiliwa, hutumwa kwa kheri na shari; haifai kuutukana, na wala haitakiwi kusema: Mwenyezi mungu aulaani upepo, au Mwenyezi Mungu auangamize upepo, Mwenyezi Mungu asiubariki upepo huu, au mfano wa hayo, bali muumini anafanya yale aliyoelekezwa na Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  5. Yanalinganishwa na upepo katika uharamu wa kushutumu na kutukana yanayohusu joto na baridi na jua na vumbi na mengineyo katika yale ambayo ni katika viumbe vya Mwenyezi Mungu na uendeshaji wake.