عن أنس وأبي هريرة رضي الله عنهما مرفوعاً: «لا يُؤْمِنُ أحدُكم حتى أَكُونَ أَحَبَّ إليه مِن وَلَدِه، ووالِدِه، والناس أجمعين».
[صحيح] - [حديث أنس -رضي الله عنه-: متفق عليه. حديث أبي هريرة -رضي الله عنه-: رواه البخاري]
المزيــد ...

Kutoka kwa Anasi na Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Hadithi Marfu'u: "Hawezi kuamini mmoja wenu mpaka niwe napendeka kwake zaidi kuliko mtoto wake, na mzazi wake, na watu wote".
Sahihi - Imepokelewa na Al-Bukhaariy

Ufafanuzi

Anatueleza Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi hii: Yakuwa haikamiliki imani ya muislamu, na wala haifikii imani ambayo ataingia nayo peponi bila adhabu, mpaka atangulize mapenzi ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- juu ya mapenzi ya mwanaye na mzazi wake na watu wote, Na hilo ni kwasababu mapenzi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu yanamaanisha: Kumpenda Mwenyezi Mungu; kwasababu Mtume ndiye mfikishaji kutoka kwake, na muongozaji katika dini yake, na mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake hayawi sawa ispokuwa kwa kutekeleza maamrisho ya sheria na kuyaepuka makatazo yake, na wala si kwa kuimba kaswida, na kufanya sherehe, na kuremba nyimbo.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Ulazima wa mapenzi ya Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- na kuyatanguliza juu ya mapenzi ya kila kiumbe.
  2. Matendo ni katika imani; kwasababu mapenzi ni katika amali za moyoni, na imekanushwa imani kwa yule ambaye Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake hatopendeka kwake kuliko vilivyotajwa.
  3. Nikuwa kukanushwa (kuwa hana imani) hakumaanishi ni kutoka katika uislamu.
  4. Nikuwa imani ya kweli ni lazima athari yake ionekana kwa mwenyewe.
  5. Ulazima wa kutanguliza mapenzi ya Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake juu ya mapenzi ya nafsi, na watoto na wazazi, na watu wote.
  6. Kujitoa fidia kwa ajili ya Mtume kwa nafsi na mali; kwasababu ni lazima utangulize mapenzi yake juu ya nafsi yako na mali zako.
  7. Nikuwa ni wajibu juu ya mtu kunusuru sunna za Mtume wa Mwenyezi Mungu, na aitoe kwaajili ya hilo nafsi yake na mali yake na nguvu zake zote; kwasababu hilo ni katika ukamilifu wa mapenzi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, na kwaajili hiyo wamesema baadhi ya wanachuoni katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika adui yako ndiye atakayekuwa mkiwa" Yaani: Anayekuchukia, wakasema: na vile vile mwenye kuchukia sheria yake; naye pia kakatikiwa hana kheri yoyote.
  8. Kufaa mapenzi ambayo ni kwaajili ya huruma na ukarimu na kutukuza; kwa kauli yake: "Nipendeke zaidi kuliko mtoto wake na mzazi wake" akathibitisha msingi wa mapenzi, na hilo ni jambo la kimaumbile wala hakuna anayelipinga.
  9. Uwajibu wa kutanguliza kauli ya Mtume Juu ya kauli ya watu wote: kwasababu katika mambo yanayoonyesha kuwa yeye anapendeka zaidi kuliko yeyote nikuwa kauli yake ni yenye kutangulizwa juu ya yeyote katika watu, hata juu ya nafsi yako.