+ -

عَنْ سَلْمَانَ الْفَارِسِيِّ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«ثَلَاثَةٌ لَا يُكَلِّمُهُمُ اللَّهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ: أُشَيْمِطٌ زَانٍ، وَعَائِلٌ مُسْتَكْبِرٌ، وَرَجُلٌ جَعَلَ اللَّهَ لَهُ بِضَاعَةً، فَلَا يَبِيعُ إِلَّا بِيَمِينِهِ وَلَا يَشْتَرِي إِلَّا بِيَمِينِهِ».

[صحيح] - [رواه الطبراني] - [المعجم الصغير: 821]
المزيــد ...

Na kutoka kwa Salmani Alfaaris -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Watu wa aina tatu hatowasemesha Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama wala hatowatakasa na watakuwa na adhabu chungu, Mzee mzinifu, na masikini jeuri, na mtu aliyemfanya Mwenyezi Mungu kuwa ndio bidhaa, hauzi ila kwa kiapo chake wala hanunui ila kwa kiapo chake".

[Sahihi] - [Ameipokea Twabraaniy]

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu aina tatu za watu, wenye kustahiki adhabu ya Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama kwa adhabu tatu, endapo hawatotubia au kusamehewa adhabu: Ya kwanza: Hatowasemesha Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama kwa sababu ya ukali wa ghadhabu yake, bali atawapuuza, au atawasemesha maneno yasiyowafurahisha na yanayoonyesha hasira yake juu yao. Ya pili: Hatowatakasa wala hatowasifia wala hatowasafisha kutokana na madhambi. Ya tatu: Watakuwa na adhabu yenye kuumiza sana Akhera. Na watu wa aina hiyo ni: Aina ya kwanza: Mtu mzima na anajiingiza katika machafu ya zinaa. Ya pili: Fakiri asiyekuwa na mali lakini pamoja na hivyo ana kiburi kwa watu. Ya tatu: Anayekithirisha kuapa kwa jina la Mwenyezi Mungu katika kuuza na kununua, analidhalilisha jina la Mwenyezi Mungu, na analifanya kuwa ndio nyenzo ya kujipatia mali.

Katika Faida za Hadithi

  1. Amesema Kadhi Iyadhi katika sababu ya adhabu hii kali: Nikuwa kila mmoja miongoni mwao alishikamana na maasi haya yaliyotajwa pamoja nakuwa yuko mbali nayo, na hapakuwa na haja ya kufanya hivyo, na udhaifu wa vishawishi vyake kwake; hata kama hakuna anayepewa udhuru wa kufanya dhambi, lakini kwa sababu hapakuwa na haja ya kutenda maasi haya yenye kukera, wala kishawishi kilichozoeleka, hii inafanana na ukaidi, na kudharau haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akaamua kumuasi si kwamba ana haja ya kufanya hivyo.
  2. Zinaa na uongo na kiburi ni katika madhambi makubwa.
  3. Kiburi: Ni kukataa haki, na kuwadharau viumbe.
  4. Tahadhari ya kukithirisha kutumia kiapo katika kuuza na kununua, na himizo la kuheshimu kiapo, na kuheshimu majina ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, amesema Mtukufu: "Na wala msifanye Mwenyezi Mungu katika viapo vyenu kuwa kisingizio cha kuacha kufanya wema" [Baqara: 224].
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kikurdi Kihausa الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama