+ -

عَن أَبي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«الْحَلِفُ مَنْفَقَةٌ لِلسِّلْعَةِ، مَمْحَقَةٌ لِلرِّبْحِ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 1606]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Kiapo hutoa bidhaa, na hufuta faida".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 1606]

Ufafanuzi

Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuapa na kukithirisha kiapo hata kama mtu akiwa mkweli katika kuuza na kununua, na akaeleza kuwa ni sababu ya kuondoka bidhaa na mzigo, lakini hilo hupunguza na kubatilisha baraka za faida na chumo, na anaweza kumpelekea Mwenyezi Mungu namna zitakazoharibu mali yake, ima kuibiwa au kuungua kuangamia au kuporwa au kuvamiwa au majanga mengine yatayoharibu mali yake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Lugha ya kifaransa Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kikurdi Kihausa Kireno Kiassam الغوجاراتية الصربية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Ukubwa wa swala la kuapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, na kwamba hakuwi ila kwa haja.
  2. Kipato cha haramu hata kama kitakuwa kingi; basi hicho kimeondolewa baraka wala hakina kheri ndani yake.
  3. Amesema Qaari: Kuondoka kwa baraka za kipato; ima kwa uharibifu unaoweza kutokea katika mali yake, au kwa kuitoa katika mambo ambayo hanufaiki nayo katika dunia au thawabu Akhera, au zikabakia kwake lakini akanyimwa kunufaika nazo, au akazirithi ambaye hatomshukuru.
  4. Amesema Nawawi: Hapa kuna katazo la kukithirisha kuapa katika biashara, kwa sababu kuapa pasina haja ni machukizo, na linaambatana hilo na kupambia bidhaa, na huenda mnunuzi akadanganyika na kiapo.
  5. Kukithirisha viapo ni upungufu wa imani, na ni upungufu wa tauhidi; kwa sababu kukithirisha viapo kuna pelekea mambo mawili: La kwanza: Kupuuza hilo na kutojali, la pili: Uongo, kwa sababu mwenye kukithiri viapo vyake huingia katika uongo, ni lazima kupunguza na kutokithirisha viapo, na ndio maana alisema Mtukufu: "Na hifadhini viapo vyenu" [Maaida: 89].