عَنْ أَنَسٍ رضي الله عنه قَالَ:
كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُكْثِرُ أَنْ يَقُولَ: «يَا مُقَلِّبَ القُلُوبِ ثَبِّتْ قَلْبِي عَلَى دِينِكَ»، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ، آمَنَّا بِكَ وَبِمَا جِئْتَ بِهِ فَهَلْ تَخَافُ عَلَيْنَا؟ قَالَ: «نَعَمْ، إِنَّ القُلُوبَ بَيْنَ أُصْبُعَيْنِ مِنْ أَصَابِعِ اللهِ يُقَلِّبُهَا كَيْفَ يَشَاءُ».
[صحيح] - [رواه الترمذي وأحمد] - [سنن الترمذي: 2140]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema:
Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akisema mara kwa mara: “Ewe Mbadilishaji nyoyo, uweke imara moyo wangu katika dini yako.” Basi nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tunakuamini wewe na ulicholeta, je unatuhofia? Akasema: "Ndio, nyoyo ziko baina ya vidole viwili vya Mwenyezi Mungu, anazigeuza kwa namna atakavyo"
[Sahihi] - - [سنن الترمذي - 2140]
Dua nyingi za Mtume rehema na amani ziwe juu yake zilikuwa ni kumuomba Mwenyezi Mungu uthabiti katika dini na utiifu, na kujiepusha na kupinda na upotofu. Anas bin Malik radhi za Allah ziwe juu yake alistaajabu kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akiiomba dua hii mara kwa mara, basi Mtume rehema na amani zimshukie akamwambia kuwa nyoyo ziko baina ya vidole viwili vya Mwenyezi Mungu, huzigeuza apendavyo, hivyo, moyo ni kituo cha imani na ukafiri, na moyo umeitwa Qalbu kwa sababu ya kugeukageuka kwake mara kwa mara, moyo hugeuka sana kuliko chungu kinapokusanyika kile kinachotokota ndani yake. Amtakaye Mwenyezi Mungu huudumisha moyo wake katika uongofu na uthabiti katika Dini, na anayemtaka Mwenyezi Mungu huugeuza moyo wake kutoka katika uongofu na kuupeleka katika upotofu.