+ -

عَن أَبي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«مَنْ قَالَ: رَضِيتُ بِاللَّهِ رَبًّا، وَبِالْإِسْلَامِ دِينًا، وَبِمُحَمَّدٍ رَسُولًا، وَجَبَتْ لَهُ الْجَنَّةُ».

[صحيح] - [رواه أبو داود] - [سنن أبي داود: 1529]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake, yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Atakayesema nimeridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola, na kuwa Uislamu ni dini, na Muhammadi kuwa Mtume, basi atastahiki kwake Papo".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Abuu Daud] - [سنن أبي داود - 1529]

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema: "Nimemridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola" na Mungu na Mlezi na Mmiliki, na bwana na Mtengenezaji, "na Uislamu" kwa hukumu zake zote kwanzia amri zake na makatazo yake "kuwa Dini" mila na sheria, itikadi na utii, "na Muhammadi kuwa Mtume" na Nabii; kwa yote aliyotumwa kwayo na akatufikishia, isipokuwa itamstahikia kwake Pepo.

Tafsiri: Lugha ya Kiindonesia Kivetenamu Kiassam الهولندية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Himizo la kusema dua hii, na kumebainishwa thawabu zinazoambatana nayo.
  2. Kumridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola, kunaambatana na mtu kutomuabudu asiyekuwa yeye Mtukufu.
  3. Kumridhia Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake kuwa Nabii na Mtume, kunaambatana na kumtii rehema na amani ziwe juu yake na kutii sunna zake.
  4. Kuridhia Uislamu kuwa dini ni kuridhia yale aliyoyachagua Mwenyezi Mungu kwa waja wake.
  5. Sunna ya kusema dua hii wakati wa shahada mbili baada kusikia Adhana, kama ilivyokuja katika riwaya zingine.
  6. Na imekuja katika hadithi nyingine sunna ya kuomba dua hii wakati wa asubuhi na jioni.