عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ:
«مَنْ قَالَ: لاَ إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، فِي يَوْمٍ مِائَةَ مَرَّةٍ، كَانَتْ لَهُ عَدْلَ عَشْرِ رِقَابٍ، وَكُتِبَتْ لَهُ مِائَةُ حَسَنَةٍ، وَمُحِيَتْ عَنْهُ مِائَةُ سَيِّئَةٍ، وَكَانَتْ لَهُ حِرْزًا مِنَ الشَّيْطَانِ يَوْمَهُ ذَلِكَ حَتَّى يُمْسِيَ، وَلَمْ يَأْتِ أَحَدٌ بِأَفْضَلَ مِمَّا جَاءَ بِهِ إِلَّا أَحَدٌ عَمِلَ أَكْثَرَ مِنْ ذَلِكَ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 3293]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Atakayesema: (Laa ilaaha illa llahu, wah-dahu laa sharika lahu, Lahul mulku, Walahul hamdu, Wahuwa alaa kulli shaini Qadiir) kwa siku mara mia moja, inakuwa kwakwe ni sawa na kuacha huru watu kumi, na anaandikiwa mema mia moja, na anafutiwa makosa mia moja, na inakuwa kwake ni kinga kutokana na Shetani kwa siku yake nzima mpaka afike jioni, na hatokuja yeyote na jambo bora zaidi kuliko atakalokuja nalo, isipokuwa yeyote atakayefanya zaidi ya alivyofanya yeye".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 3293]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema: "Hapana Mola" na hakuna muabudiwa wa haki "isipokuwa Mwenyezi Mungu, yeye pekee asiye na mshirika" katika uungu wake na ulezi wake na majina yake na sifa zake, "Ufalme ni wake" na maamuzi na mipangilio yote, "naye juu ya kila kitu ni muweza" pasina wa kumzuia wala wa kumkinga, na asiyoyataka hayawezi kuwa. Atakayesema dhikiri hii kwa siku mara mia moja, ataandikiwa ujira kutoka kwa Mwenyezi Mungu sawa na aliyeacha huru watumwa kumi, na ataandikiwa kwa maneno hayo mema mia moja na daraja Peponi, na yatafutwa kwake makosa mia moja, na yatakuwa ni kinga na kizuizi na ngome dhidi ya Shetani na upotovu wake na usaliti wake katika siku yake hiyo mpaka iingie jioni kwa kuzama jua, na hatoleta yeyote siku ya Kiyama kitu bora kuliko alichokuja nacho, isipokuwa mtu aliyefanya zaidi ya hivyo na akazidisha zaidi ya hapo.