+ -

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ رضي الله عنها أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَّمَهَا هَذَا الدُّعَاءَ:
«اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ الْخَيْرِ كُلِّهِ، عَاجِلِهِ وَآجِلِهِ، مَا عَلِمْتُ مِنْهُ وَمَا لَمْ أَعْلَمْ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ الشَّرِّ كُلِّهِ، عَاجِلِهِ وَآجِلِهِ، مَا عَلِمْتُ مِنْهُ وَمَا لَمْ أَعْلَمْ، اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ خَيْرِ مَا سَأَلَكَ عَبْدُكَ وَنَبِيُّكَ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا عَاذَ بِهِ عَبْدُكَ وَنَبِيُّكَ، اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْجَنَّةَ، وَمَا قَرَّبَ إِلَيْهَا مِنْ قَوْلٍ أَوْ عَمَلٍ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ النَّارِ، وَمَا قَرَّبَ إِلَيْهَا مِنْ قَوْلٍ أَوْ عَمَلٍ، وَأَسْأَلُكَ أَنْ تَجْعَلَ كُلَّ قَضَاءٍ قَضَيْتَهُ لِي خَيْرًا».

[صحيح] - [رواه ابن ماجه وأحمد] - [سنن ابن ماجه: 3846]
المزيــد ...

Kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimfundisha dua hii:
"Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba (unipe) kutoka katika heri zote: zile za haraka na za kuchelewa, kwa ninayo yajua na nisiyo yajua, na ninajikinga kwako kutokana na shari zote zinazokuja haraka na zinazochelewa, kwa ninayo yajua na nisiyo yajua. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba (unipe) miongoni mwa heri alizo kuomba mja wako na nabii wako, na ninajikinga kwako (uniepushe) na shari alizo jikinga kwako mja wako na nabii wako. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba pepo, na yaliyo karibu yake miongoni mwa kauli au matendo, na ninajikinga kwako kutokana na moto na yaliyo karibu na moto miongoni mwa kauli au matendo, na ninakuomba ujaalie kila hukumu utakayo hukumu kwangu iwe ni heri"

[Sahihi] - - [سنن ابن ماجه - 3846]

Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimfundisha Aisha radhi za Allah ziwe juu yake dua inayokusanya mambo mengi nayo ni maombi manne:
La kwanza: Dua inayokusanya kila aina ya kheri: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba unipe kutoka katika kheri zote" kwa ujumla wake, "Za haraka" zilizo karibu kwa wakati wake, na "za baadaye" za mbali, "Nilizozijua" katika zile ulizonifundisha, "na zile nisizozijua" katika zile zinazokuwa katika elimu yako ewe Mtukufu, Na hapa kuna kuyakabidhi mambo yote kwa Mwenyezi Mungu Mjuzi Mwenye habari na Mpole; basi Mwenyezi Mungu humchagulia muislamu kilicho bora kati ya hayo na kizuri, "Na ninajilinda" ninashikamana na ninaomba ulinzi "kwako wewe dhidi ya shari zote, zinazokuja haraka na zinazochelewa, ninazozijua na nisizozijua".
Dua ya pili: Nayo ni kinga kwa muislamu ili asichupe mipaka katika dua "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba" na ninakutaka unipe "Katika kheri alizokuomba mja wako na Nabii wako" rehema na amani ziwe juu yake, "na ninajilinda kwako" na ninajiegemeza na kushikamana "kwako kutokana na shari alizojikinga nazo mja wako na Nabii wako" rehema na amani ziwe juu yake, na hii ni dua na ni ombi kutoka kwa Mwenyezi Mungu ampe muombaji yale aliyomuomba na akayataka Nabii Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake kwa ajili ya nafsi yake, pasina kusema aina ya yale aliyoyaomba rehema na amani ziwe juu yake.
Dua ya tatu: Kuomba kuingia peponi na kujiweka mbali na moto, nalo ni ombi la kila muislamu na ndio lengo kuu la matendo yake: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba pepo" na kufauli kuipata "Na yale yanayotuweka karibu nayo miongoni mwa kauli na matendo" mema yenye kukuridhisha, "na ninajilinda kwako kutokana na moto" kiasi kwamba hakuna kukingwa na matendo machafu ila kwa upole wako, "na yale yenye kutuweka karibu nao miongoni mwa kauli na matendo" katika maasi yanayokukasirisha.
Dua ya nne: Kuomba kuridhika na kadari za Mwenyezi Mungu "na ninakuomba uyafanya maamuzi yako uliyoyapitisha yawe ni kheri" na kila jambo alilolihukumu Mwenyezi Mungu kwangu alifanye kuwa ni kheri kwangu, na ni katika dua za kuomba kuridhia hukumu ya Mwenyezi Mungu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Thai Pashto Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الرومانية Luqadda Oromaha
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Mtu anatakiwa kuifundisha familia yake yale yenye kuwanufaisha katika mambo ya dini na dunia, kama Mtume rehema na amani ziwe juu yake alivyomfundisha Aisha.
  2. Kilicho bora kwa muislamu ni kuhifadhi dua zilizopokelewa kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake; kwa sababu ni katika dua zilizokusanya kheri zote.
  3. Wanachuoni wanasema kuhusu hadithi hii: Ni hadithi iliyokusanya kila kitu katika kuomba kheri na kuomba kinga dhidi ya shari, hii ni katika maneno mafupi yenye maana pana aliyopewa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  4. Miongoni mwa sababu za kuingia peponi baada ya rehema ya Mwenyezi Mungu: Ni matendo na kauli njema.