+ -

عَن عبدِ اللهِ بن خُبَيب رضي الله عنه أنه قال:
خَرَجْنَا فِي لَيْلَةٍ مَطِيرَةٍ وَظُلْمَةٍ شَدِيدَةٍ، نَطْلُبُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ؛ يُصَلِّي لَنَا، قَالَ: فَأَدْرَكْتُهُ، فَقَالَ: «قُلْ»، فَلَمْ أَقُلْ شَيْئًا، ثُمَّ قَالَ: «قُلْ»، فَلَمْ أَقُلْ شَيْئًا، قَالَ: «قُلْ»، فَقُلْتُ: مَا أَقُولُ؟ قَالَ: «{قُلْ هُوَ اللهُ أَحَدٌ} وَالْمُعَوِّذَتَيْنِ حِينَ تُمْسِي وَتُصْبِحُ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، تَكْفِيكَ مِنْ كُلِّ شَيْءٍ».

[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي والنسائي] - [سنن الترمذي: 3575]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abdillah Bin Khubaibi Radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa yeye amesema:
Tulitoka katika usiku wa mvua kubwa na giza nene, tukimtafuta Mtume rehema na amani ziwe juu yake; ili atusalishe, anasema: Nikampata, akasema: "Sema" Nikawa sikusema kitu, kisha akasema: "Sema", Nikawa sikusema kitu, akasema: "Sema" Nikasema: Niseme nini? Akasema: "Sema Yeye ni Mwenyezi Mungu mmoja tu" na sura mbili za kinga unapofika nyakati za jioni na nyakati za asubuhi mara tatu, zitakutosheleza kila kitu".

[Sahihi] - - [سنن الترمذي - 3575]

Ufafanuzi

Anaeleza swahaba mtukufu Abdullah Bin Khubaib radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa wao walitoka katika usiku wenye mvua kubwa, na giza lilikuwa nene, kwa ajili ya kumtafuta Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake; ili awasalishe, wakamkuta, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: "Sema" Yaani: Soma, akawa hakusoma kitu, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akarejea kauli yake kwake, Abdullah akasema: Nisome nini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Soma suratul Ikhlaswi (Qul-huwallaahu ahadi), na sura mbili za kinga (Qul-Audhubirabbil-falaq), na (Qul-Audhubirabbin-naas), wakati wa jioni, na wakati wa asubuhi, mara tatu tatu, zitakuhifadhi na kila shari, na zitakukinga na kila baya.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Sunna ya kusoma Suratul Ikhlasi na sura mbili za kinga asubuhi na jioni, nakuwa sura hizo ni kinga dhidi ya kila shari.
  2. Ubora wa kusoma suratul Ikhlasi na sura mbili za kinga.