عن سعد بن عبادة رضي الله عنه أنه قال:
يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّ أُمَّ سَعْدٍ مَاتَتْ، فَأَيُّ الصَّدَقَةِ أَفْضَلُ؟، قَالَ: «الْمَاءُ»، قَالَ: فَحَفَرَ بِئْرًا، وَقَالَ: هَذِهِ لِأُمِّ سَعْدٍ.
[حسن بمجموع طرقه] - [رواه أبو داود والنسائي وابن ماجه] - [سنن أبي داود: 1681]
المزيــد ...
Kutoka kwa Sa'di bin Ubada radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yakwamba amesema:
Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mama Sa'di amefariki, ni sadaka ipi bora ya kumfanyia? Akasema: "Maji" Akasema: tukachimba kisima, na akasema: Kisima hiki ni kwa ajili ya mama Sa'di.
- - [سنن أبي داود - 1681]
Alifariki mama Sa'di bin Ubada radhi za Allah ziwe juu yake, akamuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni aina ipi bora ya sadaka ili aitoe kwa niaba ya mama yake? Akamueleza rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa sadaka bora ni maji, akachimba kisima na akakifanya kuwa sadaka kwa ajili ya mama yake.