عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عَدِيِّ بْنِ الخِيَارِ قَالَ:
أَخْبَرَنِي رَجُلَانِ أَنَّهُمَا أَتَيَا النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي حَجَّةِ الوَدَاعِ وَهُوَ يُقَسِّمُ الصَّدَقَةَ، فَسَأَلَاهُ مِنْهَا، فَرَفَّعَ فِينَا البَصَرَ وَخَفَّضَهُ، فَرَآنَا جَلْدَيْنِ، فَقَالَ: «إِنَّ شِئْتُمَا أَعْطَيْتُكُمَا، وَلَا حَظَّ فِيهَا لِغَنِيٍّ، وَلَا لِقَوِيٍّ مُكْتَسِبٍ».
[صحيح] - [رواه أبو داود والنسائي] - [سنن أبي داود: 1633]
المزيــد ...
Kutoka kwa Ubaidillah bin Adiy binil-Khiyari amesema:
Walinieleza watu wawili kuwa wao walimjia Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika Hija ya kuaga wakati akigawa sadaka, wakamuomba katika sadaka hizo, akatunyanyulia macho kisha akayashusha, akatuona ni watu shupavu wenye nguvu, akasema: "Ikiwa mtapenda nitakupeni, lakini mali hii tajiri hana fungu ndani yake wala mwenye nguvu mwenye uwezo wa kuchuma mali".
[Sahihi] - [رواه أبو داود والنسائي] - [سنن أبي داود - 1633]
Walikuja watu wawili kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika Hija ya kuaga, wakati akigawa sadaka, na wakamuomba awapatie katika sadaka hizo, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawa anawatazama mara kwa mara, ili ajue hali zao, na je, ni halali kwao kupewa sadaka au la? Akawaona ni wanaume wawili wenye nguvu, akasema: Ikiwa mtapenda nitawapa katika sadaka hizi, lakini hana fungu ndani yake mwenye mali inayomtosheleza, wala kwa mwenye uwezo wa kutafuta na kuchuma mali, hata asipokuwa na mali inayomfanya ahesabike miongoni mwa wenye uwezo.