عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«مَا مِنْ يَوْمٍ يُصْبِحُ العِبَادُ فِيهِ إِلَّا مَلَكَانِ يَنْزِلاَنِ، فَيَقُولُ أَحَدُهُمَا: اللَّهُمَّ أَعْطِ مُنْفِقًا خَلَفًا، وَيَقُولُ الآخَرُ: اللَّهُمَّ أَعْطِ مُمْسِكًا تَلَفًا».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 1442]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Hakuna siku ambayo wanaamka ndani yake waja isipokuwa kuna Malaika wawili wanateremka, anasema mmoja wao: Ewe Mwenyezi Mungu mpe mtoaji badala, na anasema mwingine: Ewe Mwenyezi Mungu mpe mzuiaji (Bahili) hasara".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 1442]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa katika kila siku inayochomozewa na Jua ndani yake kuna Malaika wawili wanateremka na kunadi, anasema mmoja wao:
Ewe Mwenyezi Mungu mpe mwenye kutoa katika njia za utiifu na kwa familia na kwa wageni na sadaka za hiyari mrejeshee na mpe badala bora kuliko kile alichotoa, na umbariki.
Na anasema mwingine: Ewe Mwenyezi Mungu mpe bahili mzuiaji uharibifu katika mali yake na uiteketeze mali yake anayoizuia na kutompa mwenye kustahiki.