عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ رضي الله عنه قَالَ:
قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ مَا النَّجَاةُ؟ قَالَ: «امْلِكْ عَلَيْكَ لِسَانَكَ، وَلْيَسَعْكَ بَيْتُكَ، وَابْكِ عَلَى خَطِيئَتِكَ».
[صحيح] - [رواه الترمذي وأحمد] - [سنن الترمذي: 2406]
المزيــد ...
Kutoka kwa Ukba bin Aamir Al-Juhaniy -radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni kupi kunusurika? Akasema: "Shika ulimi wako, na ikutoshe nyumba yako, na lia kwa ajili ya makosa yako".
[Sahihi] - - [سنن الترمذي - 2406]
Ukba bin Aamiri alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu sababu za muumini kuokoka katika dunia na Akhera?
Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Shikamana na mambo matatu:
La kwanza: Hifadhi ulimi wako katika yale yasiyokuwa na kheri ndani yake, na kuzungumza kila shari, na usitamke ila la kheri.
La pili: Baki nyumbani kwako ili umuabudu Mwenyezi Mungu katika nyakati za faragha, na ujishughulishe na kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ibada, na jitenge nyumbani kwako na fitina.
La tatu: Lia na ujute na utubie kwa yale uliyoyatenda katika madhambi.