+ -

عَنْ ‌أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ:
قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لِعَمِّهِ: «قُلْ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، أَشْهَدُ لَكَ بِهَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ»، قَالَ: لَوْلَا أَنْ تُعَيِّرَنِي قُرَيْشٌ، يَقُولُونَ: إِنَّمَا حَمَلَهُ عَلَى ذَلِكَ الْجَزَعُ لَأَقْرَرْتُ بِهَا عَيْنَكَ. فَأَنْزَلَ اللهُ: {إِنَّكَ لا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَكِنَّ اللهَ يَهْدِي مَنْ يَشَاءُ } [القصص: 56].

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 25]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimwambia baba yake mdogo: "Sema: Laa ilaaha illa llahu, nitakutolea ushuhuda wa kusilimu kwa maneno hayo siku ya Kiyama" Akasema: Ningetamka kama si kuogopea matusi ya Makuraishi wanasema kulichompelekea kusema maneno hayo ni kuogopa kifo, kama si hivyo ningeingiza furaha moyoni mwako, basi Mwenyezi Mungu akateremsha: "Hakika wewe huwezi kumuongoza umtakaye lakini Mwenyezi Mungu humuongoza amtakaye" (suratul Qaswas: 56)

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 25]

Ufafanuzi

Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimtaka Abuu Twalib ambaye ni baba yake mdogo akiwa katika kilevi cha mauti, atamke neno Laa ilaaha illa llahu, ili amuombee utetezi kwa neno hilo siku ya Kiyama, na amtolee ushuhuda wa kusilimu kwake, akakataa kutamka shahada kwa kuogopea kuwa Makuraishi watamtukana na watamsema kuwa: Amesilimu kwa sababu ya kuogopa mauti na unyonge! Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Kama si huko kuogopa ningeingiza furaha katika moyo wako kwa kutamka kwako shahada na mauti yangekufika kwa namna ambayo ungeiridhia! basi akateremsha Mwenyei Mungu Aya ambayo inajulisha kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hamiliki uongofu wa kuukubali uislamu, bali Mwenyezi Mungu aliyetukuka peke yake humuwezesha amtakaye. Na kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake anawaongoza viumbe kwa ufahamu na kuwawekea wazi na kuwaongoza pamoja na kuwaita kwenye njia iliyonyooka.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga Luqadda Asariga الأوزبكية الأوكرانية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Haki huwa haiachwi kwa sababu ya maneno ya watu.
  2. Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anamiliki uongofu wa ufahamishaji na uelekezaji na siyo uongofu wa kukubaliwa.
  3. Ni katika sheria kumtembelea Kafiri akiwa mgonjwa kwa ajili ya kumlingania katika uislamu.
  4. Pupa ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika kulingania kuelekea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa hali yoyote.