عَنْ ‌قَتَادَةَ رحمه الله قال:
حَدَّثَنَا ‌أَنَسُ بْنُ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ رَجُلًا قَالَ: يَا نَبِيَّ اللهِ كَيْفَ يُحْشَرُ الْكَافِرُ عَلَى وَجْهِهِ؟ قَالَ: «أَلَيْسَ الَّذِي أَمْشَاهُ عَلَى الرِّجْلَيْنِ فِي الدُّنْيَا قَادِرًا عَلَى أَنْ يُمْشِيَهُ عَلَى وَجْهِهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ؟» قَالَ قَتَادَةُ: بَلَى وَعِزَّةِ رَبِّنَا.

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 6523]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Qatadah -Mwenyezi Mungu amrehemu amesema:
Alitusimulia Anas Bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa Mtu mmoja alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu vipi kafiri atafufuliwa akitembea kwa uso wake? Akasema: "Hivi yule aliyemfanya atembee kwa miguu miwili hawezi kumfanya atembee kwa uso wake siku ya Kiyama?" Akasema Qatadah: Kwa nini asiweze, ninaapa kwa utukufu wa Mola wetu anaweza kufanya hivyo.

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake] - [Swahiih Al Bukhaariy - 6523]

Ufafanuzi

Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- vipi atafufuliwa Kafiri akitembea kwa uso wake siku ya Kiyama? Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akasema: Hivi Mwenyezi Mungu aliyemfanya atembee kwa miguu miwili hapa Duniani hawezi kumfanya atembee kwa uso wake siku ya Kiyama?! Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu.

Katika Faida za Hadithi

  1. Udhalili utampata Kafiri siku ya Kiyama na atatembea kwa uso wake.
Kuonyesha Tarjama
Lugha: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Ziada (65)