+ -

عَنْ ‌عَائِشَةَ رضي الله عنها:
أَنَّ رَجُلًا قَعَدَ بَيْنَ يَدَيِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ، إِنَّ لِي مَمْلُوكِينَ يَكْذِبُونَنِي وَيَخُونُونَنِي وَيَعْصُونَنِي، وَأَشْتُمُهُمْ وَأَضْرِبُهُمْ، فَكَيْفَ أَنَا مِنْهُمْ؟ قَالَ: «يُحْسَبُ مَا خَانُوكَ وَعَصَوْكَ وَكَذَّبُوكَ وَعِقَابُكَ إِيَّاهُمْ، فَإِنْ كَانَ عِقَابُكَ إِيَّاهُمْ بِقَدْرِ ذُنُوبِهِمْ كَانَ كَفَافًا، لَا لَكَ وَلَا عَلَيْكَ، وَإِنْ كَانَ عِقَابُكَ إِيَّاهُمْ دُونَ ذُنُوبِهِمْ كَانَ فَضْلًا لَكَ، وَإِنْ كَانَ عِقَابُكَ إِيَّاهُمْ فَوْقَ ذُنُوبِهِمُ اقْتُصَّ لَهُمْ مِنْكَ الْفَضْلُ»، قَالَ: فَتَنَحَّى الرَّجُلُ فَجَعَلَ يَبْكِي وَيَهْتِفُ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَمَا تَقْرَأُ كِتَابَ اللهِ: {وَنَضَعُ الْمَوَازِينَ الْقِسْطَ لِيَوْمِ الْقِيَامَةِ فَلا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْئًا}، الْآيَةَ»، فَقَالَ الرَّجُلُ: وَاللهِ يَا رَسُولَ اللهِ، مَا أَجِدُ لِي وَلهُمْ شَيْئًا خَيْرًا مِنْ مُفَارَقَتِهِمْ، أُشْهِدُكَ أَنَّهُمْ أَحْرَارٌ كُلُّهُمْ.

[ضعيف] - [رواه الترمذي] - [سنن الترمذي: 3165]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-:
Ya kuwa mtu mmoja alikaa mbele ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa hakika mimi nina watu niliowamiliki, wakati mwingine wananidanganya na wananifanyia hiyana na wanakwenda kinyume na amri zangu, nahuwa nawatia adabu kwa kuwatukana na kuwapiga, hivyo naulizia kuwa ni vipi itakuwa hali yangu kwa kuwafanyia hayo?Akasema: "Watahesabiwa kwa hiyana waliyokufanyia na kukuasi na kukudanganya, na itahesabiwa adhabu yako uliyowapa basi ikiwa adhabu uliyowapa ipo sawa na makosa yao basi itatosha na hapatakuwa na chochote kwako wala kwao, na ikiwa adhabu uliyowapa ni ya chini kulingana na kosa walilofanya basi utalipwa na utazidishiwa kwenye malipo yako, na ikiwa umewaadhibu zaidi ya walivyokosea yatapunguzwa kutoka kwako malipo ya ziada" Akasema: Basi yule bwana alijitenga na akawa analia kwa sauti ya juu, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamwambia: "Hivi husomi katika kitabu cha Mwenyezi Mungu aliposema: "Na Sisi tutaweka Mizani ya uadilifu siku ya Kiyama na hakuna nafsi yoyote itakayodhulumiwa kwa chochote", mpaka mwisho wa Aya, yule bwana akasema: Nakuapia ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sijaona kheri iliyopo kati yangu na yao zaidi ya kuwaachia huru, na ninakupa ushuhuda kuwa wao wote kuanzia sasa wako huru".

[Dhaifu] - [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy] - [سنن الترمذي - 3165]

Ufafanuzi

Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akishitakia kuhusu matendo ya Watumwa wake, Watumwa hao wanamdanganya na kumfanyia hiyana katika amana, na wanafanya ghushi katika miamala, na wanakwenda kinyume na maelekezo yake, naye huwatia adabu kwa kuwatukana na kuwapiga, hivyo akaulizia kuhusu hali yake itakavyokuwa siku ya Kiyama, basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Watahesabiwa kwa kile walichokufanyia hiyana na kwenda kinyume na maelekezo yako na kukudanganya na wewe utahesabiwa ulivyo waadhibu, basi ikiwa adhabu uliyowapa itakuwa sawa na makosa yao basi hutokuwa na kosa lolote, na ikiwa adhabu uliyowapa ni ndogo ikilinganishwa na kosa walilofanya basi ni jambo zuri utalipwa na utazidishiwa katika malipo yako, na ikiwa adhabu uliyowapa ni zaidi ya walichokifanya, basi utaadhibiwa na malipo yako uliyozidishiwa yatachukuliwa na watapewa wao, basi yule bwana akakaa pembeni akawa analia kwa sauti ya juu, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamwambia: "Hivi husomi katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu aliposema: "Na Sisi tutaweka Mizani ya uadilifu siku ya Kiyama na hakuna nafsi yoyote itakayodhulumiwa kwa chochote, hata kama jambo hilo litakuwa na uzito sawa na punje ya Hardal tutalileta Nasi tunatosha kuwa wajuzi wa hisabu" (Al-Anbiyaa 47), hivyo basi hatodhulumiwa mtu yoyote siku ya kiyama, na kipimo cha watu kitakuwa cha uadilifu, yule bwana akasema: Nakuapia ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sijaona kheri iliyopo kati yangu na wao zaidi ya kuwaacha huru ninakupa ushuhuda kuwa wao wote kuanzia hivi sasa wako huru kwa ajili ya Mwenyezi Mungu; kwa kuogopea hesabu na adhabu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Ki ighori Kibangali Kituruki Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kivetenamu Kihausa Kimalayo Kitelguu Burmese Thai Pashto Kiassam السويدية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية Luqadda kiniya ruwadiga التشيكية Luqadda malgaashka الفولانية Kiitaliano Luqadda kinaadiga اليونانية الأوزبكية الأوكرانية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Ukweli wa Swahaba katika kuwaacha huru watumwa wake kwa kuogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu.
  2. Inafaa kumuadhibu dhalimu ikiwa adhabu hiyo itakuwa sawa na makosa yake au kumwadhibu adhabu ndogo ikilinganishwa na kosa lake, ama kumzidishia adhabu ni haramu na haifai.
  3. Himizo la kuamiliana vizuri na watumishi na watu madhaifu.
Ziada