‌عن عَلِيٍّ قَالَ: إِنِّي كُنْتُ رَجُلًا إِذَا سَمِعْتُ مِنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَدِيثًا نَفَعَنِي اللهُ مِنْهُ بِمَا شَاءَ أَنْ يَنْفَعَنِي بِهِ، وَإِذَا حَدَّثَنِي رَجُلٌ مِنْ أَصْحَابِهِ اسْتَحْلَفْتُهُ، فَإِذَا حَلَفَ لِي صَدَّقْتُهُ، وَإِنَّهُ حَدَّثَنِي ‌أَبُو بَكْرٍ، وَصَدَقَ أَبُو بَكْرٍ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«مَا مِنْ رَجُلٍ يُذْنِبُ ذَنْبًا، ثُمَّ يَقُومُ فَيَتَطَهَّرُ، ثُمَّ يُصَلِّي، ثُمَّ يَسْتَغْفِرُ اللهَ، إِلَّا غَفَرَ اللهُ لَهُ»، ثُمَّ قَرَأَ هَذِهِ الْآيَةَ: {وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنْفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ} [آل عمران: 135].

[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي والنسائي في الكبرى وابن ماجه وأحمد]
المزيــد ...

Kutoka kwa Ally amesema: Hakika mimi nilikuwa ni mtu kila nikisikia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hadithi Mwenyezi Mungu ananinufaisha kwa hadithi hiyo kwa kiasi alichotaka kuninufaisha, na akinihadithia yeyote katika Masahaba zake ninamuapisha, akiniapia ninamuamini, na siku moja alinihadithia Abubakari, na Abubakari akasema ukweli, akasema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Hakuna mtu yeyote atakayetenda dhambi, kisha akasimama akajitwaharisha, kisha akaswali, kisha akamuomba Allah msamaha, isipokuwa Mwenyezi Mungu humsamehe", Kisha akasoma aya hii: "Na wale ambao wakifanya machafu au wakizidhulumu nafsi zao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakaomba msamaha kutokana na madhambi yao" [Al-Imran: 135].

Sahihi - Imepokelewa na Abuu Daud

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hakuna mja yeyote atakayetenda dhambi, akatawadha vizuri, kisha akasimama na akaswali rakaa mbili kwa nia ya kuomba toba kutokana na dhambi lake hili, kisha akamuomba Allah msamaha, isipokuwa Mwenyezi Mungu humsamehe. Kisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasoma kauli yake Mtukufu: "Na wale ambao wakitenda dhambi kubwa au wakizidhulumu nafsi zao kwa kutenda dhambi chini ya hizo, wanaikumbuka ahadi ya Mwenyezi Mungu ya malipo mema kwa wanaomtii na malipo mabaya kwa wanaomuasi na wanaelekea kwa Mola wao hali ya kutubia wakawa wanamuomba Awasamehe madhambi yao na wakawa wana yakini kwamba hapana anayesamehe madhambi isipokuwa Mwenyezi Mungu. Na wao kwa sababu hiyo hawaendelei kwenye maasi, na wao wanajua kwamba wakitubia Mwenyezi Mungu Atawakubalia toba yao". [Surat Al-Imran: 135].

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Kichina Kifursi Kihindi Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kimalayo Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Himizo la kuswali kisha kuomba msamaha baada ya kutenda dhambi.
  2. Upana wa msamaha wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kukubali kwake toba na msamaha.