+ -

عَنْ ‌عَائِشَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهَا قَالَتْ:
تَلَا رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ هَذِهِ الْآيَةَ: {هُوَ الَّذِي أَنْزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ، وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلَّا اللَّهُ، وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِنْ عِنْدِ رَبِّنَا وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ} [آل عمران: 7]. قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «فَإِذَا رَأَيْتِ الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ فَأُولَئِكَ الَّذِينَ سَمَّى اللهُ، فَاحْذَرُوهُمْ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 4547]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
Alisoma Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake Aya hii :{Yeye ndiye ambaye alikuteremshia kitabu hiki ndani yake kuna Aya muhkam -zilizo wazi- aya hizo ambazo ndiyo msingi wa kitabu hiki na zipo nyingine zinatatiza, wale ambao nyoyoni mwao kuna upotofu watafuata zile zenye kutatiza kwa kutaka kufitinisha na kutaka kujua uhakika wa maana yake, na hakuna ajuaye uhakika wa maana yake isipokuwa Mwenyezi Mungu, na wale wabobezi katika elimu wanasema tumeziamini zote zimetoka kwa Mola wetu na hawakumbuki isipokuwa wenye akili} (Al- imaraan 7) Anasema Aisha: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Ikiwa utawaona wenye kufuata Aya zenye kutatiza basi hao ndiyo ambao Mwenyezi Mungu amewataja katika aya"

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 4547]

Ufafanuzi

Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alisoma aya hii: {Huwal ladhii Anzala alaikal kitaab minhu aayaatu muhkamaatun hunnaa ummul kitaab,wa ukharu mutashaabihaat,fa-ammal ladhiina fii quluubihim zaighun fayattabiuuna maatashaabaha minhu ib-tighaal fitnat wabtighaa taawiilihi,wamaa yaalamu taawilahu illa llahu warrasikhuuna fil ilmi yaquuluuna aamanna bihi kullu min in-di rabbinaa wamaa yaddhakkaru illa ulul al-baab}, Ndani ya aya hii Mwenyezi Mungu Mtukufu amefahamisha kuwa yeye ndiye aliyeteremsha Qur'ani kwa Mtume wake Qur'ani ambayo kuna aya zinazofahamika kwa uwazi, hukumu zake zinafahamika na hazitatizi, na aya hizo ni msingi wa kitabu hiki na ndiyo marejeo yake, nayo Qur'ani ndiyo marejeo inapotokea kutofautiana, na katika Qur'ani hiyo kuna aya zingine zinachukuwa maana zaidi ya moja maana zake zinawatatiza baadhi ya watu, au wanadhani kuwa kati ya aya na aya nyingine kuna mgongano, kisha akaweka wazi Mwenyezi Mungu namna watu wanavyozifanyia kazi aya hizi, basi wale ambao katika nyoyo zao kuna upotofu wa kuiwacha haki huziwacha aya zilizokuwa wazi, na wanachukuwa zile zenye kutatiza wakitaka kuibua utata na kuwatatiza watu, na kufanya hivyo wanataka kwa kutumia maana hiyo iafikiane na matamanio ya nafsi zao, ama wale ambao wamebobea kwenye elimu wanaujua utata huu, na wanazirudisha kwenye maana zilizo wazi na wanaziamini kuwa aya hizo zimetoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na haiwezekani zikapingana lakini hilo hawalikumbuki wala kupata mawaidha isipokuwa wale wenye akili iliyo salama, kisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamwambia mama wa waumini Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa ikiwa atawaona wenye kufuata aya zenye kutatiza basi hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu amewataja katika maneno yake aliposema: {Basi wale ambao katika nyoyo zao kuna maradhi} basi tahadhari nao na wala usiwasikilize.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف البلغارية Luqadda Asariga اليونانية الأوزبكية الأوكرانية الجورجية اللينجالا المقدونية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Al-muhkam katika aya za Qur'ani: Ni zile ambazo ni nyepesi kuzifahamu maana zake zipo wazi, na zenye kutatiza ni zile zenye kuchukua zaidi ya maana moja na zinahitajia uchunguzi wa kina na ufahamu.
  2. Kuchukua tahadhari ya kutochanganyikana na watu waliopotoka, na watu wazushi na wenye kuleta mambo yenye kutatiza kwa ajili ya kuwapoteza watu na kuwatia mashaka.
  3. Katika kumalizia aya kwa maneno yake Mwenyezi Mungu Mtukufu "Na hawakumbuki isipokuwa wenye akili" Inaashiria kuwapinga wapotofu na kuwasifia waliojikita katika elimu, yaani asiyekumbuka wala kupata mawaidha, na akafuata matamanio ya nafsi yake huyo si miongoni mwa wenye kutumia akili.
  4. Kufuata mambo yenye kutatiza ni sababu ya kuupotosha moyo.
  5. Ni wajibu kuzirudisha aya ambazo maana zake zinatatiza na hazifahamiki maana zake, katika aya ambazo maana yake ni nyepesi kufahamika.
  6. Mwenyezi Mungu Mtukufu amezifanya baadhi ya aya kuwa ni nyepesi na zingine ni zenye kutatiza; Ili awajaribu watu na kuwapambanua wenye imani na watu waliopotea.
  7. Kwa kutokea aya zenye kutatiza katika Qur'ani: Ni kudhihirisha ubora wa maulamaa kuliko watu wengine, na kuifahamisha akili kuhusu mapungufu yake; ili ijisalimishe kwa muumba wake na ikubali kushindwa kwake.
  8. Ubora wa kujikita katika elimu na ulazima wa kudumu katika elimu.
  9. Na maulamaa wa tafsiri kwenye kusimama katika neno (Allah) katika maneno yake aliposema {Wamaa ya'alamu taawilahuu illa llahu warraasikhuuna fil ilmi} kuna kauli mbili, kwa yule atakayesimama katika neno (Allah), basi yanakuwa makusudio ya neno Taawiil ni ujuzi wa uhakika wa kitu kwa namna ambayo hakuna njia ya kuujua, kama vile jambo linalohusu roho na kiyama katika mambo ambayo Mwenyezi Mungu ameyaficha katika elimu yake, na wale wabobezi katika elimu wao wanaziamini na wanaegemeza uhakika wake kwa Mwenyezi Mungu, hivyo basi wanajisalimisha na wanasalimika, na mwenye kupitiliza bila ya kusimama kwenye neno( Allah) basi inakuwa maana ya neno Taawili ni tafsiri na kuweka wazi, hivyo inakuwa Mwenyezi Mungu anajua na waliobobea katika elimu vilevile wanajua, hivyo wanakuwa ni wenye kuziamini na wana zirudisha kwenye aya zilizo nyepesi.