+ -

عن ابن شماسة المهري قال: حَضَرنَا عَمرو بن العاص رضي الله عنه وهُو فِي سِيَاقَةِ الْمَوتِ، فَبَكَى طَوِيلاً، وَحَوَّلَ وَجهَهُ إِلَى الجِدَارِ، فَجَعَلَ ابنَهُ، يقول: يَا أَبَتَاهُ، أَمَا بَشَّرَكَ رسُول الله -صلَّى الله عليه وسلَّم- بكَذَا؟ أمَا بشَّركَ رسول الله -صلَّى الله عليه وسلَّم- بِكَذَا؟ فَأَقبَلَ بِوَجهِهِ، فقَالَ: إِنَّ أَفضَلَ مَا نُعِدُّ شَهَادَةُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ الله، وَأَنَّ مُحَمَّدًا رسولُ الله، إِنِّي قَدْ كُنتُ عَلَى أَطْبَاقٍ ثَلاَثٍ: لَقَدْ رَأَيتُنِي وَمَا أَحَدٌ أَشَدَّ بُغْضًا لِرَسُولِ الله -صلَّى الله عليه وسلَّم- مِنِّي، وَلاَ أَحَبَّ إِلَيَّ مِنْ أَنْ أَكُونَ قَدْ اسْتَمْكَنْتُ مِنْهُ فَقَتَلْتُهُ، فَلَوْ مُتُّ عَلَى تِلْكَ الحَالِ لَكُنْتُ مِنْ أَهْلِ النَّارِ، فَلَمَّا جَعَلَ اللهُ الإِسْلاَمَ فِي قَلْبِي أَتَيتُ النَبيَّ -صلَّى الله عليه وسلَّم-، فَقُلتُ: ابْسُطْ يَمِينَكَ فَلِأُبَايِعُكَ، فَبَسَطَ يَمِينَهُ فَقَبَضْتُ يَدِي، فقال: «مَا لَكَ يَا عَمرُو؟» قُلتُ: أَرَدْتُ أَنْ أَشْتَرِطَ، قال: «تَشْتَرِطُ مَاذَا؟» قُلتُ: أَنْ يُغْفَرَ لِي، قال: «أَمَا عَلِمتَ أَنَّ الإِسْلاَمَ يَهْدِمُ مَا كَانَ قَبْلَهُ، وَأَنَّ الهِجْرَةَ تَهْدِمُ مَا كَانَ قَبْلَهَا، وَأَنَّ الحَجَّ يَهْدِمُ مَا كَانَ قَبْلَهُ؟» وَمَا كَان أَحَدٌ أَحبَّ إِلَيَّ مِنْ رسُول الله -صلَّى الله عليه وسلَّم- وَلاَ أَجَلَّ فِي عَينِي مِنْهُ، وَمَا كُنْتُ أُطِيقُ أَنْ أَمْلَأَ عَينِي مِنْهُ؛ إِجْلاَلاً لَهُ، وَلَوْ سُئِلْتُ أَنْ أَصِفَهُ مَا أَطَقْتُ؛ لِأَنِّي لَمْ أَكُنْ أَمْلَأُ عَينِي مِنْهُ، وَلَوْ مِتُّ عَلَى تِلْكَ الحَالِ لَرَجَوْتُ أَنْ أَكُونَ مِنْ أَهْلِ الجَنَّةِ، ثُمَّ وَلِينَا أَشْيَاءَ مَا أَدْرِي مَا حَالِي فِيهَا؟ فَإِذَا أَنَا مِتُّ فَلاَ تَصْحَبْنِي نَائِحَةٌ وَلاَ نَارٌ، فَإِذَا دَفَنْتُمُونِي، فَشُنُّوا عَلَيَّ التُرَابَ شَنًّا، ثُمَّ أَقِيمُوا حَولَ قَبرِي قَدْرَ مَا تُنْحَرُ جَزُور، وَيُقْسَمُ لَحْمُهَا، حتَّى أَسْتَأْنِسَ بِكُم، وَأَنْظُر مَا أُرَاجِعُ بِهِ رُسُلَ رَبِّي.
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa bin Shammasa Al Mihriy Amesema:Tulifika kwa Amru bin Aaswi naye akiwa katika safari ya kifo, akalia kwa muda mrefu, na akageuza uso wake kuelekea ukutani, mwanaye akaanza kusema, Ewe baba yangu, kwani hakukubashiria Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake kwa jambo kadhaa (yaani pepo)? kwani hakukubashiria Mtume-Rehema na Amani ziwe juu yake kwa jambo kadhaa? akageuka kwa uso wake, kisha akasema: Hakika jambo bora katika yale tunayoyaandaa ni kushuhudia kuwa Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Hakika mimi nilikuwa katika hali za aina tatu: Nilijikuta mimi kuwa hakuna anayemchukia kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuliko mimi, Na hakuna kitu nilichotamani zaidi kama kumtia mikononi ili nimuue, basi lau ningekufa katika hali hiyo ningekuwa ni katika watu wa motoni, Basi Mwenyezi Mungu alipouweka Uislamu moyoni mwangu, nilimuendea Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- Kisha nikasema: Nyoosha mkono wako wa kulia ili nikupe utiifu wangu kwako, basi akanyoosha mkono wake wa kulia nikakunja mkono wangu, akasema: "Umekuwaje wewe Amru?" Nikasema: Nilitaka niweke sharti kwanza, akasema: "Unaweka sharti la kitu gani?" Nikasema: Nisamehewe, akasema: "Hivi hukujua kuwa uislamu hufuta makosa yaliyokuwa kabla yake, na kuwa kuhama kunafuta makosa yaliyokuwa kabla yake, nakuwa Hija hufuta makosa yaliyokuwa kabla yake?" Kuanzia hapo hapakuwa tena na yeyote niliyempenda zaidi kuliko Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- wala niliyemuheshimu zaidi machoni mwangu kuliko yeye, Na sikuwa naweza kumtazama kwa macho yangu; kwasababu ya kumuheshimu, na hata kama ningeombwa nimsifie nisingeweza; kwasababu mimi sikuwa naweza kumtazama kwa macho yangu, na lau ningekufa katika hali hiyo ningetaraji kuwa miongoni mwa watu wa peponi, Kisha tukatawala mambo ambayo mpaka sasa sijui hali yangu ndani yake? Basi ikiwa nitakufa nisifuatwe na maombolezo wala moto, na mkinizika, basi nimwagieni udongo kidogo kidogo, kisha bakini kaburini kwangu kwa kiasi cha muda wa kuweza kumchinja ngamia na kumchuna, na kugawanywa nyama yake, ili nijiliwaze kwenu, na nisubiri nini nitawajibu wajumbe wa Mola wangu.
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim]

Ufafanuzi

Imekusanya hadithi ya Amru bin Aaswi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- maudhui za habari njema na pongezi za kheri ndani ya kisa, na muhtasari wa kisa hiki kitukufu: Nikuwa yeye walimfikia baadhi ya jamaa zake naye akiwa katika safari ya kifo, akalia kilio kikubwa, na akageuza uso wake upande wa ukutani -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-, naye akiwa katika safari ya kifo ataachana na dunia, mwanaye akasema kumwambia: Unalilia nini na haliyakuwa tayari alishakubashiria pepo Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-? Akasema: Ewe mwanangu, hakika mimi nilikuwa katika hali tatu, kisha akazitaja hali hizi tatu: Yakuwa yeye alikuwa akimchukia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- chuki ya hali ya juu, nakuwa duniani hapakuwa na mtu anayemchukia zaidi kama yeye, mpaka Mwenyezi Mungu akauingiza Uislamu ndani ya moyo wake akaja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-, akasema: Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu: Nyoosha mkono wako ili nikupe utiifu wangu juu ya uislamu, na alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ni mwenye tabia nzuri kuliko watu wote akanyoosha mkono wake, lakini Amri bin Aaswi akakunja mkono wake, si kwasababu ya kiburi, lakini ni kwasababu ya kuyathibitisha yale atakayoyaeleza, akasema kumwambia: "Umekuaje?" Akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika mimi ninaweka sharti -yaani juu ya kusilimu- Akasema: "Ni kitu gani unaweka sharti?" Akasema: Ninaweka sharti kuwa anisamehe Mwenyezi Mungu mimi yaliyopita katika ukafiri miongoni mwa madhambi. Hii ndio ilikuwa hamu yake kubwa -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Anaweka sharti kuwa Mwenyezi Mungu amsamehe, alidhani kuwa Mwenyezi Mungu hatomsamehe katika yale aliyokuwa nayo nyuma, Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akasema kumwambia-: "Hivi hukujua kuwa uislamu unabomoa(unafuta) yaliyokuwa kabla yake, na kuwa kuhama kunabomoa yaliyokuwa kabla yake, nakuwa Hija inabomoa yaliyokuwa kabla yake?". Mambo matatu. Ama Uislamu unabomoa yaliyokuwa kabla yake kwa ushahidi wa kitabu kitukufu: Amesema Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka: "Waambie wale waliokufuru: "kama wataacha (yale mabaya waliyokuwa nayo) watasamehewa yaliyopita, na wakiyarudia (tutawatesa kama tulivyo watesa wao mara zilizopita) Imekwisha kuwapitia wao mifano (ya mambo yaliyowapata) watu wa zamani". Na kuhama: atakapohama mtu kutoka katika mji wake ambao anaishi ndani yake, na katika mji wa kikafiri hilo linafuta yaliyokuwa kabla yake. Na hija: inabomoa yaliyokuwa kabla yake; kwa kauli ya Mtume- Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Atakayehiji akawa hakufanya mabaya na akawa hakufanya machafu atarudi kama siku alivyozaliwa na mama yake". Hapo akampa utiifu -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- na akampenda Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- mapenzi makubwa mpaka akawa ni mtu anayependeka zaidi kwake, na mpaka akawa hawezi kumkazia jicho; kwa kumuheshimu yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- Ametakasika mwenye kuzigeuza nyoyo! jana alikuwa akimchukia chuki kubwa mpaka anatamani apate nafasi ili amuuwe, na sasa hivi hawezi hata kunyanyua jicho lake kumtazama; kwasababu ya kumuheshimu, na wala hawezi hata kumuelezea kwasababu hawezi kumtazama akamaliza, kiasi ambacho hakuweza kumjua vizuri; kwasababu ya mapenzi yake kwake -Rehema na Amani ziwe juu yake- Anasema -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-. Laiti angelikufa katika hali ya kwanza; basi angelikuwa ni katika watu wa motoni: Anasema: Na lau ningelikufa katika hali ile yaani hali ya pili; ningetaraji kuwa miongoni mwa watu wa peponi, hebu tazama alivyojipa uwezekano, amejihakikishia kuwa laiti angelikufa katika hali ya kwanza; angelikuwa miongoni mwa watu wa motoni, Ama hali ya pili kutokana na hofu yake kubwa amesema: Laiti ningelikufa katika hali hii basi ningetaraji kuwa miongoni mwa watu wa peponi, na hakusema: Ningekuwa ni miongoni mwa watu wa pepo; kwasababu ushuhuda wa kuingia peponi ni jambo gumu. Kisha yeye baada ya hapo akasimamia mambo -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-, alisimamia madaraka na uongozi, na yakatokea yaliyotokea katika kisa cha vita vya Muawiya na wengineo, na Amru bin Aaswi alikuwa anafahamika kwa waarabu kuwa ni katika waarabu wajanja na werevu mno, basi anasema: ninahofia kwa haya yaliyotokea kwangu baada ya ile hali ya katikati huenda yakawa yameyazingira matendo yangu. Kisha akatoa usia -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa yeye atakapokufa asifuatwe na maombolezo, na muombolezaji: Ni mwanamke anayemuomboleza maiti, na analia kilio kinachofanana na mlio wa punda, na akaamrisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- watakapomzika wabakie katika kaburi lake kiasi cha kuchinja ngamia mmoja, na kugawika nyama yake, mpaka awajibu wajumbe wa Mola wake nao ni Malaika wale wanaomjia maiti anapozikwa, Maiti anapozikwa humjia Malaika wawili na wanamkalisha ndani ya kaburi lake, na wanamuuliza maswali matatu: wanasema: Nani Mola wako? Na ni ipi dini yako? Na ni nani Nabii wako?. Akaamrisha Amru bin Aaswi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- watu wake wasimame juu yake kiasi cha kuchinjwa ngamia na kugawanywa nyama yake; ili ajiliwaze kupitia wao, Na hii inaonyesha kuwa maiti huwa anawahisi watu wake, na imethibiti kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa maiti husikia nyayo za viatu vyao, wanapoondoka baada ya kumzika, nyayo za viatu za kimya kimya anazisikia maiti wanapoondoka baada ya kumzika. Na imethibiti kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi ambayo daraja yake ni (Hasan) kuwa yeye alikuwa anapomzika maiti anasimama juu yake, na Anasema: "Muombeeni msamaha ndugu yenu, na muombeeni kuthubutu; kwani yeye wakati huu anaulizwa", Hivyo ni sunna na inapendeza anapozikwa maiti mtu asimame juu ya kaburi lake na aseme: Ewe Mwenyezi Mungu mpe uthubutu (umakinifu), Ewe Mwenyezi Mungu mpe uthubutu (umakinifu), Ewe Mwenyezi Mungu mpe uthubutu (umakinifu), Ewe Mwenyezi Mungu msamehe; kwasababu Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa anapotoa salamu basi anatoa salamu mara tatu, na anapoomba anaomba mara tatu. Kilichopo nikuwa mtoto wa Amru bin Aaswi alisema kumwambia: Alikupa habari njema wewe Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ya kuingia peponi, na hii ni sehemu ya kujipa bishara njema na kujipongeza kwayo.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno
Kuonyesha Tarjama