+ -

عَنِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ:
أَلَسْتُمْ فِي طَعَامٍ وَشَرَابٍ مَا شِئْتُمْ؟ لَقَدْ رَأَيْتُ نَبِيَّكُمْ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَمَا يَجِدُ مِنَ الدَّقَلِ مَا يَمْلَأُ بِهِ بَطْنَهُ.

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2977]
المزيــد ...

Kutoka kwa Nuuman bin Bashiri radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema:
Hivi leo hii nyinyi si mnapata chakula na kinywaji mkitakacho? Kwa hakika mimi nilimuona Nabii wenu rehema na amani ziwe juu yake inafika mahala hapati hata tende mbovu ya kutosha kujaza tumbo lake.

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2977]

Ufafanuzi

Anaeleza Nuuman bin Bashiri radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, maisha waliyonayo watu miongoni mwa neema, na kwamba wao muda wote wana uhakika wa chakula na kinywaji kwa kiwango watakacho, kisha akaeleza kuhusu hali ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kwamba alikuwa hapati katika tende mbovu kiasi cha kujaza tumbo lake kutokana na njaa.

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumebainishwa hali aliyokuwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kuipa nyongo Dunia.
  2. Himizo la kuipa nyongo Dunia, na kuipunguza kwa kadiri iwezekanavyo, na kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  3. Kuwakumbusha watu neema walizonazo, na kuwahimiza wamshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema hizo.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kiassam الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama