عَن أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«يُسَلِّمُ الرَّاكِبُ عَلَى المَاشِي، وَالمَاشِي عَلَى القَاعِدِ، وَالقَلِيلُ عَلَى الكَثِيرِ».
وَلِلبُخَارِي: «يُسَلِّمُ الصَّغِيرُ عَلَى الكَبِيرِ، وَالمَارُّ عَلَى القَاعِدِ، وَالقَلِيلُ عَلَى الكَثِيرِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 6232]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Amsalimie aliyepanda anayetembea, na anayetembea aliyekaa, na wachache kwa wengi"
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 6232]
Ameelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika adabu za kutoleana salamu kati ya waislamu "Assalaam alaikum warahmatullaahi wabarakaatuh". Mdogo amsalimie mkubwa, na aliyepanda amsalimie anayetembea kwa miguu, na anayetembea kwa mguu amsalimie aliyekaa, na idadi ndogo wawasalimie idadi kubwa.