+ -

عَنْ صَفْوَانَ بْنِ مُحْرِزٍ قَالَ: قَالَ رَجُلٌ لِابْنِ عُمَرَ رضي الله عنهما كَيْفَ سَمِعْتَ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: فِي النَّجْوَى؟ قَالَ: سَمِعْتُهُ يَقُولُ:
«يُدْنَى الْمُؤْمِنُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مِنْ رَبِّهِ عَزَّ وَجَلَّ، حَتَّى يَضَعَ عَلَيْهِ كَنَفَهُ، فَيُقَرِّرُهُ بِذُنُوبِهِ، فَيَقُولُ: هَلْ تَعْرِفُ؟ فَيَقُولُ: أَيْ رَبِّ أَعْرِفُ، قَالَ: فَإِنِّي قَدْ سَتَرْتُهَا عَلَيْكَ فِي الدُّنْيَا، وَإِنِّي أَغْفِرُهَا لَكَ الْيَوْمَ، فَيُعْطَى صَحِيفَةَ حَسَنَاتِهِ، وَأَمَّا الْكُفَّارُ وَالْمُنَافِقُونَ، فَيُنَادَى بِهِمْ عَلَى رؤُوسِ الْخَلَائِقِ هَؤُلَاءِ الَّذِينَ كَذَبُوا عَلَى اللهِ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 2768]
المزيــد ...

Kutoka kwa Swafwan bin Muhrizi amesema: Mtu mmoja alisema kumwambia bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao, ulimsikia akisema nini Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu kunong'ona? Akasema: nilimsikia akisema:
"Atasogezwa muumini siku ya Kiyama karibu na Mola wake Mlezi Aliyetakasika na Kutukuka, kisha atamuwekea pazia lake, hapo atamuonyesha wazi madhambi yake ili akiri, kisha atasema: Je wayajua? Atasema: Ndiyo Mola wangu ninayajua, atasema: Basi hakika mimi nilikusitiri madhambi haya ulipokuwa duniani, na mimi ninakusamehe madhambi hayo leo hii, hapo atapewa faili la mema yake, na ama makafiri na wanafiki, wataitwa hadharani mbele ya kadamnasi, (kisha patasemwa) hawa ndio waliompinga Mwenyezi Mungu"

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 2768]

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu Mwenyezi Mungu kunong'ona na mja wake muumini siku ya Kiyama, akasema:
Atasogezwa muumini siku ya Kiyama karibu na Mola wake Mlezi kisha atamuwekea pazia lake la kumkinga na watu walioko katika kisimamo, hakuna atakayeona katika pazia hilo zaidi yake, hapo atamwambia:
Je walijua dhambi fulani na fulani... atamtaka akiri madhambi yake yaliyokuwa kati ya mja na Mola wake Mlezi.
Naye atasema: Ndiyo, ewe Mola Mlezi.
Mpaka atakapofadhaika muumini na kuogopa, Mtukufu atamwambia: Mimi niliyasitiri kwako madhambi haya duniani, na mimi leo hii ninayasamehe kwa ajili yako, hapo atapewa faili la mema yake.
Na ama kafiri na mnafiki wataitwa mbele ya kadamnasi: Hawa ndiyo waliomkadhibisha Mola wao Mlezi, basi tambueni kuwa laana za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya madhalimu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Thai Pashto Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda yuruuba
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Fadhila za Mwenyezi Mungu na rehema zake kwa waumini kwa kuwasitiri duniani na Akhera.
  2. Himizo la kumsitiri muumini kwa kadiri iwezekanavyo.
  3. Matendo ya waja yote anayakusanya Mola Mlezi wa waja, yeyote atakayekuta kheri basi na amshukuru Mwenyezi Mungu, na atakayekuta kinyume na hivyo basi asimlaumu yeyote ila nafsi yake, naye atakuwa chini ya maamuzi ya Mwenyezi Mungu.
  4. Amesema bin Hajari: Hadithi nyingi zimeonyesha kuwa waumini wenye maasi siku ya Kiyama watakuwa katika sehemu mbili: Sehemu ya kwanza: Ni yule ambaye maasi yake yatakuwa kati yake na Mola wake Mlezi, ikaonyesha hadithi ya bin Omari kuwa sehemu hii pia itakuwa imegawanyika katika sehemu mbili: Kuna sehemu ambayo maasi yake yatakuwa yamesitiriwa duniani, haya ambayo anayasitiri Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama, na sehemu hii ndiyo iliyotajwa katika hadithi, na sehemu nyingine: Ni wale ambao maasi yao yatakuwa wazi, ikaonyesha maana ya hadithi hii kuwa watakuwa kinyume na hao. Na sehemu ya pili: Ni wale ambao maasi yao yatakuwa kati yao na waja, nao wamegawanyika sehemu mbili pia: Kuna sehemu mabaya yao yatazidi mema yao, hawa watadondoka motoni na watatoka kwa utetezi, na sehemu nyingine: Ni wale yaliolingana sawa mabaya yao na mema yao, hawa hawatoingia peponi mpaka kipite kisasi baina yao.