عن أنس رضي الله عنه مرفوعاً: «يَتْبَعُ الميتَ ثلاثةٌ: أهْلُه ومَالُه وعَمَلُه، فيرجع اثنان ويَبْقى واحد: يرجع أهْلُه ومَالُه، ويبقى عَمَلُه».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Yanamfuata maiti mambo matatu: familia yake na mali yake na matendo yake, vinarudi vitu viwili na kinabakia kimoja: wanarudi familia yake na mali yake, na yanabakia matendo yake"
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Maana ya hadithi: anapokufa mwanadamu wanamfuata wenye kumsindikiza, wanamfuata watu wake wanamsindikiza mpaka kaburini kwake, na zinamfuata mali zake: yaani watumwa wake na wafanyakazi wake na mamluki (anao wamiliki) wake, na yanamfuata pamoja naye matendo yake, vinarudi viwili, na yanabakia matendo yake, ikiwa kama ni ya kheri basi itakuwa kheri na ikiwa ni ya shari pia itakuwa shari.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno
Kuonyesha Tarjama