+ -

عَنْ أَبِي بَرْزَةَ الأَسْلَمِيِّ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«لَا تَزُولُ قَدَمَا عَبْدٍ يَوْمَ القِيَامَةِ حَتَّى يُسْأَلَ عَنْ عُمُرِهِ فِيمَا أَفْنَاهُ، وَعَنْ عِلْمِهِ فِيمَ فَعَلَ، وَعَنْ مَالِهِ مِنْ أَيْنَ اكْتَسَبَهُ وَفِيمَ أَنْفَقَهُ، وَعَنْ جِسْمِهِ فِيمَ أَبْلَاهُ».

[صحيح] - [رواه الترمذي] - [سنن الترمذي: 2417]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Barza Al Aslamia -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Hautonyanyuka unyayo wa mja siku ya Kiyama mpaka aulizwe kuhusu umri wake aliumaliza katika mambo yapi? Na kuhusu elimu yake aliifanyia kazi katika nini? Na kuhusu mali yake ni wapi aliichuma? Na aliitoa katika mambo gani? Na kuhusu mwili wake aliumaliza katika mambo yapi?"

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy] - [سنن الترمذي - 2417]

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa hatovuka mtu yeyote kisimamo cha hesabu siku ya Kiyama kwenda peponi au motoni mpaka aulizwe kuhusu mambo kadhaa:
La kwanza: Maisha yake aliyatumia na kuyamaliza katika nini?
La pili: Elimu yake, je aliitafuta kwa lengo la kupata radhi za Allah? na je aliifanyia kazi? na je aliifikisha kwa wenye kustahiki?
La tatu: Mali yake ni wapi aliichuma, je ni katika halali au haramu? Na aliitoa katika mambo gani, ni katika yale yenye kumridhisha Allah au yenye kumchukiza?.
La nne: Mwili wake na nguvu zake na afya yake na ujana wake, aliutumia na kuumaliza katika mambo gani?

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية التشيكية Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Himizo la kutumia fursa ya uhai katika yale yenye kumridhisha Allah Mtukufu.
  2. Neema za Allah kwa waja ni nyingi, na atamuuliza kila mmoja kuhusu neema aliyoishi nayo, hivyo anatakiwa aiweke kila neema ya Allah katika yale yenye kumridhisha.