عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«مَنْ كَانَتْ لَهُ مَظْلَمَةٌ لِأَخِيهِ مِنْ عِرْضِهِ أَوْ شَيْءٍ فَلْيَتَحَلَّلْهُ مِنْهُ اليَوْمَ، قَبْلَ أَلا يَكُونَ دِينَارٌ وَلاَ دِرْهَمٌ، إِنْ كَانَ لَهُ عَمَلٌ صَالِحٌ أُخِذَ مِنْهُ بِقَدْرِ مَظْلَمَتِهِ، وَإِلَمْ تَكُنْ لَهُ حَسَنَاتٌ أُخِذَ مِنْ سَيِّئَاتِ صَاحِبِهِ فَحُمِلَ عَلَيْهِ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 2449]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake:
"Atakayekuwa na dhuluma yoyote ya ndugu yake kama heshima au chochote, basi na wamalizane leo hii, kabla ya wakati ambao hapatakuwa na Dinar wala Dirham, ikiwa atakuwa na amali njema basi zitachukuliwa kwake kwa kiasi cha dhuluma yake, na akiwa hana mema basi yatachukuliwa maovu ya mwenye haki na atabebeshwa yeye".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 2449]
Amemuamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kutumbukia katika dhuluma ya ndugu yake Muislamu katika heshima, au mali, au damu, basi amuombe aliyemdhulumu amsamehe madamu bado yuko Duniani, kabla haijafika siku ya Kiyama, kiasi ambacho Dinar ya dhahabu wala Dirham ya fedha haitofaa kitu kwa kumlipa aliyemdhulumu ili aikomboe nafsi yake; kwani kisasi siku hiyo kitakuwa kwa matendo mema na mabaya; kiasi kwamba aliyedhulumiwa atachukua kutoka katika mema ya aliyemdhulumu kwa kiwango cha dhuluma yake alichodhulumiwa, ikiwa dhalimu hatokuwa na mema basi yatapunguzwa maovu ya aliyedhulumiwa na kubebeshwa dhalimu kwa kiwango cha dhuluma yake.