عن جرير بن عبد الله رضي الله عنه مرفوعاً: «مَنْ لا يَرْحَمِ النَّاسَ لا يَرْحَمْهُ اللهُ».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...
Kutoka kwa Jariri bin Abdillah Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Asiyewahurumia watu hatomuhurumia Mwenyezi Mungu".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Asiyewahurumia watu Mwenyezi Mungu Mtukufu hamuhurumii, na makusudio ya watu: watu ambao wanastahiki huruma na wanaostahiki hifadhi na mfano wao, na ama makafiri wanaotupiga vita hao hawahurumiwi, bali wanauwawa kwasababu Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema katika kumsifu Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- na maswahaba zake (Ni wakali kwa makafiri wanahurumiana wao kwa wao) Suratul-Fat-hi: 29.