عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«نِعْمَتَانِ مَغْبُونٌ فِيهِمَا كَثِيرٌ مِنَ النَّاسِ: الصِّحَّةُ وَالفَرَاغُ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 6412]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Neema mbili wamepoteza thamani yake watu wengi: Afya na wakati".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 6412]
Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu neema mbili kubwa miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu kuwa wanapata hasara ndani yake watu wengi, kiasi kwamba wanazitumia mahali pasipostahiki; kwani mwanadamu zikikusanyika kwake neema ya afya na wakati, akazidiwa na uvivu wa kufanya ibada basi kapata hasara; na ndio hali ya watu wengi, na akiutumia muda wake na afya yake katika kumtii Mwenyezi Mungu basi atakuwa kapata faida; hii ni kwa sababu dunia ndio shamba la Akhera, na wakati hufuatiwa na shughuli, na afya hufuatiwa na maradhi, na lau kusingekuwa na chochote zaidi ya uzee basi ungetosha.