عَنْ أَسْمَاءَ بِنْتِ أَبِي بَكْرٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، قَالَتْ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«إِنِّي عَلَى الحَوْضِ حَتَّى أَنْظُرَ مَنْ يَرِدُ عَلَيَّ مِنْكُمْ، وَسَيُؤْخَذُ نَاسٌ دُونِي، فَأَقُولُ: يَا رَبِّ مِنِّي وَمِنْ أُمَّتِي، فَيُقَالُ: هَلْ شَعَرْتَ مَا عَمِلُوا بَعْدَكَ، وَاللَّهِ مَا بَرِحُوا يَرْجِعُونَ عَلَى أَعْقَابِهِمْ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 6593]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Asmaa Bint Abii Bakari-Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao wote na baba yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake:
"Kwa hakika mimi nitakuwa kwenye Birika langu namtazama kila mwenye kuja kwangu kunywa, na kuna watu watafukuzwa, na nitasema: Ewe Mola wangu huyu anatokana na mimi na ni katika umma wangu, basi ataambiwa: Hivi unajua waliyoyafanya baada yako? Namuapia Mwenyezi Mungu, hawakuacha kurudi nyuma na kutoka katika dini yao."
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 6593]
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa siku ya Kiyama yeye atakuwa kwenye Birika lake ili amuone kila mwenye kuja kwenye Birika katika watu wa umma wake. Na watachukuliwa watu wakiwa karibu na Mtume -Amani iwe juu yake- basi atasema: Ewe Mola wangu hao ni wangu na nikatika umma wangu, Basi kutasemwa: Je unajua walichofanya baada ya wewe kuachana nao? Namuapia Mwenyezi Mungu hawakuwacha kurudi nyuma na kutoka katika dini yao, hivyo basi hao siyo watu wako wala si katika umma wako.