عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رضي الله عنهما قَالَ: قالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«حَوْضِي مَسِيرَةُ شَهْرٍ، مَاؤُهُ أَبْيَضُ مِنَ اللَّبَنِ، وَرِيحُهُ أَطْيَبُ مِنَ المِسْكِ، وَكِيزَانُهُ كَنُجُومِ السَّمَاءِ، مَنْ شَرِبَ مِنْهَا فَلاَ يَظْمَأُ أَبَدًا».

[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Amrou -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Birika langu ukubwa wake ni sawa na mwendo wa mwezi mzima, maji yake ni meupe kuliko maziwa, na harufu yake ni nzuri kuliko ya Miski, Vikombe vyake ni kama idadi ya nyota za mbinguni, yeyote atakaye kunywa kwenye birika hilo hatopatwa na kiu milele"

Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Ametoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yeye atakuwa na Birika siku ya Kiyama urefu wa Birika hilo ni sawa na mwendo wa miguu wa mwezi mzima, na upana wake hivyo hivyo, Na kuwa maji yake ni meupe kulio maziwa, Na kuwa harufu yake ni nzuri kuliko harufu ya Miski, Na Mabirika yake ni mfano wa nyota za mbinguni kwa wingi wake, Atakaye kunywa katika Mabirika hayo hatopatwa na kiu milele.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Kibangali Kichina Kifursi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Birika la Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mkusanyiko mkubwa wa maji wanaokwenda kunywa humo waislamu miongoni mwa watu wa umma wake siku ya kiyama.
  2. Kupata neema kwa mwenye kunywa katika Birika na kwa hivyo hatopata kiu milele.