عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«يَقْبِضُ اللَّهُ الأَرْضَ، وَيَطْوِي السَّمَوَاتِ بِيَمِينِهِ، ثُمَّ يَقُولُ: أَنَا المَلِكُ، أَيْنَ مُلُوكُ الأَرْضِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 4812]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Ataikamata Mwenyezi Mungu ardhi, na ataikunja mbingu kwa mkono wake wa kulia kisha atasema: Mimi ndiye Mfalme; wako wapi wafalme wa ardhi?"
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 4812]
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu Mtukufu ataikamata Ardhi na kuikusanya, na ataikunja Mbingu kwa mkono wake wa kulia na aikunjekunje na aiondoe na aimalize, kisha asema: Mimi ndiye Mfalme, wako wapi wafalme wa Ardhini?!