عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«لَا تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى يَتَقَارَبَ الزَّمَانُ، فَتَكُونَ السَّنَةُ كَالشَّهْرِ، وَيَكُونَ الشَّهْرُ كَالْجُمُعَةِ، وَتَكُونَ الْجُمُعَةُ كَالْيَوْمِ، وَيَكُونَ الْيَوْمُ كَالسَّاعَةِ، وَتَكُونَ السَّاعَةُ كَاحْتِرَاقِ السَّعَفَةِ الْخُوصَةُ».

[صحيح] - [رواه أحمد]
المزيــد ...

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Sala na amani ziwe juu yake-:
"Hakitosimama kiyama mpaka zama zikaribiane, mwaka utakuwa kama mwezi, na mwezi utakuwa kama wiki, na wiki kama siku, na siku kama saa, na saa itakuwa kama kuungua kwa jani kavu la mtende".

Sahihi - Imepokelewa na Ahmad

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa miongoni mwa alama za Kiyama ni kukaribiana zama. Mwaka utapita kama mwezi unavyopita, Na mwezi utapita kama inavyopita wiki, Na wiki itapita kama inavyopita siku. Na siku itapita kama inavyopita saa moja, Na saa itapita upesi kama linavyochomwa jani kavu la mtende.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Kichina Kifursi Kihindi Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kimalayo Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Miongoni mwa alama za Kiyama ni kushuka kwa baraka katika zama au uharaka wake.