عَنْ سُفْيان بنِ عَبْدِ اللهِ الثَّقَفِيّ رضي الله عنه قال:
قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ، قُلْ لِي فِي الْإِسْلَامِ قَوْلًا لَا أَسْأَلُ عَنْهُ أَحَدًا غَيْرَكَ، قَالَ: «قُلْ: آمَنْتُ بِاللهِ، ثُمَّ اسْتَقِمْ».
[صحيح] - [رواه مسلم وأحمد] - [مسند أحمد: 15416]
المزيــد ...
Kutoka kwa Sufiani bin Abdillah Al-Thaqafi Radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Nieleze ndani ya Uislamu kauli ambayo sitomuuliza yeyote zaidi yako, akasema: "Sema: Nimemuamini Mwenyezi Mungu, kisha kuwa na msimamo".
[Sahihi] - - [مسند أحمد - 15416]
Swahaba Sufiani bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake alimuomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amfundishe kauli iliyokusanya maana nzima ya Uislamu ili ashikamane nayo na wala hatomuuliza yeyote zaidi yake? Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Sema: Nimempwekesha Mwenyezi Mungu, na nimemuamini kuwa yeye ndiye Mola wangu na Mungu wangu na Muumba wangu na muabudiwa wangu wa haki aisye na mshirika wake, kisha awe mtiifu katika sheria za Mwenyezi Mungu kwa kutekeleza faradhi za Mwenyezi Mungu na kuacha maharamisho ya Mwenyezi Mungu na adumu katika hilo.