عَنِ ابْنِ عُمَرَ رضي الله عنهما عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ:
«مَثَلُ الْمُنَافِقِ، كَمَثَلِ الشَّاةِ الْعَائِرَةِ بَيْنَ الْغَنَمَيْنِ تَعِيرُ إِلَى هَذِهِ مَرَّةً وَإِلَى هَذِهِ مَرَّةً».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2784]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake-amesema:
"Mfano wa mtu mnafiki, ni kama Mbuzi mwenye kutangatanga baina ya makundi mawili ya Mbuzi, wakati mwingine huwa na kundi hili na wakati mwingine huwa na kundi lile."
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2784]
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hali za wanafiki, na kuwa mnafiki ni kama Mbuzi mwenye kutangatanga na asiyejua afuate kundi gani la Mbuzi, wakati mwingine huenda kundi hili na wakati mwingine huenda na kundi lingine, Wanafiki hutangatanga baina ya imani na ukafiri, hivyo hawapo na waumini kwa wazi wazi wala kwa kujificha, wala hawapo na makafiri kwa wazi wala kwa kujificha, bali kwa muonekano wa nje wanaonekana wapo na waumini, na kwa ndani (kwa siri) wapo kwenye shaka na kutanga tanga, wakati mwingine, na wakati mwingine wanaelemea kwa hawa na wakati mwingine kwenye kundi hili.