عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ رضي الله عنهما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«إِنَّ الْإِيمَانَ لَيَخْلَقُ فِي جَوْفِ أَحَدِكُمْ كَمَا يَخْلَقُ الثَّوْبُ الْخَلِقُ، فَاسْأَلُوا اللَّهَ أَنْ يُجَدِّدَ الْإِيمَانَ فِي قُلُوبِكُمْ».
[صحيح] - [رواه الحاكم والطبراني] - [المستدرك على الصحيحين: 5]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Umar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Hakika Imani huoza na kudhoofika kwenye mwili wa mmoja wenu kama inavyooza nguo mpya kwa kukaa muda mrefu, basi muombeni Mwenyezi Mungu aifanye Imani kuwa mpya kwenye nyoyo zenu."
[Sahihi] - - [المستدرك على الصحيحين - 5]
Anatoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Imani huoza katika moyo wa muislamu na inachakaa kama inavyochakaa nguo mpya kwa kutumika muda mrefu; Na kuoza huko ni kwa sababu ya udhaifu katika ibada, au kwa sababu ya kufanya maasi na kuzama kwenye matamanio. Basi anatoa muongozo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa tumuombe Mwenyezi Mungu Mtukufu azifanye kuwa mpya imani zetu, kwa kutekeleza mambo ya wajibu na kuzidisha kumtaja Mwenyezi Mungu na kumuomba msamaha.