عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ أَنْ تُؤْتَى رُخَصُهُ، كَمَا يُحِبُّ أَنْ تُؤْتَى عَزَائِمُهُ».
[صحيح] - [رواه ابن حبان] - [صحيح ابن حبان: 354]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Kwa hakika Mwenyezi Mungu anapenda ichukuliwe ruhusa yake katika kufanya yaliyo mepesi, kama vile anavyopendelea kwa waja wake kufanya mambo yake aliyowawajibishia kuyafanya".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Ibnu Hibaan] - [صحيح ابن حبان - 354]
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: kuwa Mwenyezi Mungu anapenda ziendewe ruhusa zake ambazo ameziweka, ikiwemo kufanya wepesi katika hukumu na ibada, na kufanya wepesi kwenye ibada kwa aliyekalifishwa na sheria ikiwa ni kwa dharura- kama vile kupunguza swala na kuikusanya wakati wa safari. Kama ambavyo Mwenyezi Mungu anapenda yafanywe mambo yake ya wajibu, kwa sababu amri ya Mwenyezi Mungu katika kufuata ruhusa na kutekeleza wajibu yote ni sawa.