عَنْ حَكِيمِ بْنِ حِزَامٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، قَالَ:
قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَرَأَيْتَ أَشْيَاءَ كُنْتُ أَتَحَنَّثُ بِهَا فِي الجَاهِلِيَّةِ مِنْ صَدَقَةٍ أَوْ عَتَاقَةٍ، وَصِلَةِ رَحِمٍ، فَهَلْ فِيهَا مِنْ أَجْرٍ؟ فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَسْلَمْتَ عَلَى مَا سَلَفَ مِنْ خَيْرٍ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 1436]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Hakiim Bin Hizaam -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni upi mtazamo wako katika mambo ambayo nilikuwa nikifanya ibada kupitia mambo hayo kabla ya kuwa muislamu, miongoni mwa sadaka, au kumwacha huru mtumwa, au kuunganisha udugu, je katika mambo hayo kuna malipo? Basi akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: " Umekwisha pokea malipo yako kutokana na mema uliyoyatanguliza".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 1436]
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kafiri anaposilimu hulipwa kwa mema aliyokuwa akiyafanya kabla ya kusilimu miongoni mwa sadaka au kuacha huru mtumwa au kuunganisha udugu.