عَنْ جَابِرٍ رضي الله عنه قَالَ:
أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَجُلٌ فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ، مَا الْمُوجِبَتَانِ؟ فَقَالَ: «مَنْ مَاتَ لَا يُشْرِكُ بِاللهِ شَيْئًا دَخَلَ الْجَنَّةَ، وَمَنْ مَاتَ يُشْرِكُ بِاللهِ شَيْئًا دَخَلَ النَّارَ»
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 93]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema:
Mtu mmoja alimjia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nini maana ya wawili wenye kustahiki? Akasema: "Yeyote atakaye kufa hali ya kuwa hamshirikishi Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia peponi, na atakaye kufa akiwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia motoni"
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 93]
Mtu mmoja alimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo mawili: ambayo yanasababisha kuingia peponi na yanayo sababisha kuingia motoni? Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akamjibu kuwa mambo ambayo yanamsababishia mtu kupata pepo ni kuwa afe mtu hali yakuwa anamuabudu Mwenyezi Mungu peke yake na wala hamshirikishi na kitu chochote. na kuwa mambo ambayo yanapelekea kuingia motoni, ni kuwa afe mtu hali yakuwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote, na anamuwekea Mwenyezi Mungu washirika na vifananishwa katika uungu wake na uumbaji wake na katika majina yake na sifa zake.