عَنْ مُعَاذٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، قَالَ:
كُنْتُ رِدْفَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى حِمَارٍ يُقَالُ لَهُ عُفَيْرٌ، فَقَالَ: «يَا مُعَاذُ، هَلْ تَدْرِي حَقَّ اللَّهِ عَلَى عِبَادِهِ، وَمَا حَقُّ العِبَادِ عَلَى اللَّهِ؟»، قُلْتُ: اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: «فَإِنَّ حَقَّ اللَّهِ عَلَى العِبَادِ أَنْ يَعْبُدُوهُ وَلا يُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا، وَحَقَّ العِبَادِ عَلَى اللَّهِ أَنْ لا يُعَذِّبَ مَنْ لا يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا»، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ أَفَلاَ أُبَشِّرُ بِهِ النَّاسَ؟ قَالَ: «لا تُبَشِّرْهُمْ، فَيَتَّكِلُوا».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 2856]
المزيــد ...
Kutoka kwa Muadhi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema:
Nilikuwa nimepanda Punda nyuma ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Punda akiitwa Ufairu, akasema Mtume: "Ewe Muadhi hivi unazijua haki za Mwenyezi Mungu kwa waja wake na zipi haki za waja kwa Mwenyezi Mungu?" Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wanajua zaidi, akasema: " Basi tambua kuwa haki za Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni wamuabudu yeye na wala wasimshirikishe na kitu chochote, na haki za waja kwa Mwenyezi Mungu asimwaadhibu yeyote ambaye hajamshirikisha yeye na chochote" Basi nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hivi kwanini nisiwape watu habari hii? Akasema Mtume: "Usiwape habari hii kwani watabweteka".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 2856]
Anaziweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- haki za Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na haki za waja kwa Mwenyezi Mungu, na kuwa haki za Mwenyezi Mungu kwa waja ni kuwa wamuabudu yeye peke yake na wala wasimshirikishe yeye na kitu chochote. Na kuwa haki za waja kwa Mwenyezi Mungu ni kutowaadhibu wenye kumpwekesha ambao hawamshirikishi yeye na chochote. Kisha Muadhi akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hivi kwa nini nisiwape watu habari hii njema ili wafurahi kwa jambo hili bora? Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamkataza kwa kuogopea kuwa watategemea habari hiyo.