عَنْ أَنَسٍ رضي الله عنه قَالَ:
جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ، مَا تَرَكْتُ حَاجَّةً وَلَا دَاجَّةً إِلَّا قَدْ أَتَيْتُ، قَالَ: «أَلَيْسَ تَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللهِ؟» ثَلَاثَ مَرَّاتٍ. قَالَ: نَعَمْ، قَالَ: «فَإِنَّ ذَلِكَ يَأْتِي عَلَى ذَلِكَ».
[صحيح] - [رواه أبو يعلى والطبراني والضياء المقدسي] - [الأحاديث المختارة للضياء المقدسي: 1773]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema:
Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi sijaacha dhambi yoyote wala maasi yoyote isipokuwa nimeyafanya, akasema: "Hivi wewe hautamki neno la shahada "Ash-hadu an-laa ilaaha illa llahu wa anna Muhamadan rasuulullah?" Akarudia mara tatu. Akasema: Ndiyo, akasema: "Kwa hakika tamko hilo hufuta makosa hayo yote."
[Sahihi] - - [الأحاديث المختارة للضياء المقدسي - 1773]
Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akasema: @Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi sijaacha dhambi yoyote wala maasi yoyote madogo wala makubwa isipokuwa nimeyafanya, je mimi nitakuwa ni mwenye kusamehewa? Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema kumwambia: Hivi wewe hautamki neno la shahada "Ash-hadu an-laa ilaha illa llahu wa anna Muhamadan rasuulullah? Akarudia kumwambia hivyo mara tatu, Basi akajibu: Ndiyo nashuhudia, Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akampa habari ya ubora na utukufu wa shahada mbili na namna inavyofuta makosa, na kuwa toba hufuta makosa yaliyopita.